loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

NHC kujenga miji midogo 3

Miradi hiyo ambayo imezinduliwa juzi itafanya mikoa ya Arusha na Dar es Salaam kuwa na muonekano wa kisasa na wa kuvutia zaidi baada ya kukamilika.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Nehemiah Mchechu katika jukwaa la uwekezaji lililoandaliwa na shirika hilo ambalo liliwashirikisha baadhi ya wakuu wa mikoa na wadau wengine.

Mchechu alisema kuna miradi midogo ya ujenzi wa nyumba lakini kuna miradi ya ujenzi wa miji midogo ambayo ndiyo wamejikita kuijenga.

Alisema katika mikakati yao wana aina tatu kubwa za ujenzi ambao ni wa nyumba za bei nafuu, ujenzi wa makazi wanayoyabomoa na ujenzi wa miji midogo.

Katika uzinduzi huo walizindua ujenzi wa miji ya Usa River, Safari iliyopo Arusha na wa Salama Creeck wa Kigamboni Dar es Salaam.

Aidha, alisema miji mingine wanayoifanyia kazi ambayo iko katika mipango ya mwisho ni miji sita.

Alisema miongoni mwa miji hiyo ni ‘Up-Town Kawe’, Kunduchi Range na Buguruni ambayo wanatarajia mpaka kufikia mwakani mipango yake itakuwa imemalizika.

Alisema kwa mradi wa Salama- Creeck, Kigamboni wanategemea utatumiwa na wakazi 25,000, Usa River pia wakazi 25,000 na mji wa Safari ambao ni mkubwa utakaliwa na watu 40,000.

Waziri wa ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka alisema kuwa serikali inaliamini shirika hilo kwani kwa kipindi kifupi limeweza kuleta mabadaliko makubwa sana.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali ...

foto
Mwandishi: Katuma Masamba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi