loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ni shida uzinduzi fiesta Mwanza

Ni shida uzinduzi fiesta Mwanza

Burudani ilianza kuonekana hasa baada ya kundi la wasanii maarufu kuwasili jijini Mwanza. Hawa si wengine, ni wasanii maarufu wanaotamba hivi sasa kwa muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Fleva na Hip hop.

Baada ya kuwasili jijini Mwanza walipata fursa ya kutembelea maeneo kadhaa kikiwemo kiwanda cha bia ya Serengeti, Serengeti Breweries, ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo kwa mwaka huu kupitia bia yao ya Serengeti.

Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la Serengeti la Fiesta, Sebastian Maganga anasema kuwa fiesta ya mwaka huu ambayo iko kiburudani zaidi, pia ina lengo la kusambaza upendo kwa Watanzania wenye kupenda burudani. Maganga anasema kwa mwaka huu imezinduliwa jijini Mwanza kutokana na umuhimu wa kipekee kwa wakazi wa Jiji la Mwanza.

Anasema miaka 10 iliyopita (mwaka 2004), Fiesta ya kwanza kutoka nje ya Jiji la Dar es Salaam iliyokuwa na kaulimbiu ya ‘Utamaduni unaendelea’ ilizinduliwa jijini Mwanza.

“Hivyo tumeona ni vyema kwa mwaka huu turudishe heshima kwa wakazi wa Jiji la Mwanza, ambao tarehe kama ya leo, mwaka 2004 Fiesta ya kwanza tuliizindua hapa Rock City, hivyo tumeona kwa mwaka huu tuwape heshima wakazi wa Rocky City kwa kuizindulia fiesta hapa tukiadhimisha miaka kumi”, anaeleza Maganga.

Anasema kwa kipindi cha miaka 10, Watanzania wameshuhudia namna tamasha la fiesta lilivyoendelea kusambaza upendo ambapo limewajumuisha wasanii wadogo na wakubwa. Na safari hii, anasema Serengeti fiesta imeongeza miji na itakuwa miji 18 badala ya 14 ya mwaka jana. Anaitaja miji iliyoongezwa kuwa ni Songea, Bukoba, Kahama, Songea na Rukwa.

Anasema kuwa fiesta ya mwaka huu, iko kiburudani zaidi hasa kwa kuzingatia kaulimbiu ya mwaka huu, ambayo ni ‘Sambaza upendo’. Anaongeza kuwa fiesta ya mwaka huu iko katika mtazamo wa kuwaunganisha na kuwaleta pamoja Watanzania wenye kupenda burudani, wakizungumza mambo ya utaifa na kujenga uzalendo kupitia burudani.

“Hivyo fiesta ya mwaka huu itakuwa na muda mrefu zaidi wa kutoa burudani, kupitia kwa wasanii mahiri ambao baadhi yao wametokana na uwepo wa Tamasha la Fiesta, hivyo Prime Time Promotion kwa kushirikiana na Serengeti Breweries inajivunia mafanikio makubwa ya kuwepo kwa tamsha hili,” anaeleza mwenyekiti huyo wa waratibu.

Kwa mujibu wa Maganga, msanii Young Killer aliyekuwa miongoni mwa wasanii wachanga waliokuwa kivutio katika tamasha hilo jijini Mwanza, ni miongoni mwa waliobuliwa na fiesta.

“Leo tuko hapa Mwanza tukiizindua rasmi fiesta, huku tukijivunia kuwa na msanii mchanga Young Killer ambaye ni tunda la fiesta. “Na kwa namna ya pekee ninawashukuru Serengeti Breweries kwa kutudhamini kwa awamu nyingine tena na hivyo kutuwezesha kusambaza upendo kwa Watanzania kupitia burudani ya fiesta,” anasema.

Anasema tamasha la mwaka huu ni la aina yake kutokana na kuwa na wasanii mahiri wa ndani na nje. Baadhi ya wasanii mahiri watakaotumbuiza mwaka huu na waliopata fursa ya kutoa burudani kwa wakazi wa Jiji la Mwanza ni Nassib Abdul ‘Diamond Platinum’, Ney wa Mitego, Young D, Mr Blue, Barakah Da Prince, Chegge na Temba, Madee, Makomando, Stamina, Young Killer, Vanessa Mdee na wengine kibao.

Tamasha hilo lilitanguliwa na mashindano ya Serengeti Fiesta Soka Bonanza 2014, ambayo yalishirikisha soka timu za baa mbalimbali za jijini Mwanza. Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweries (SBL), Ephraim Mafuru alisema uongozi wa SBL kwa kushirikiana na wadau wengine, umechukua mawazo na changamoto mpya, ukilinganisha na matamasha ya fiesta ya miaka ya nyuma ili kuyaboresha zaidi.

“Katika fiesta ya mwaka huu, itakuwa na wasanii wakubwa, ambako ninawaomba Watanzania popote watakapokuwa wajitokeze kwa wingi sio tu kuja kunywa bia ya Serengeti, bali wafike kufurahia burudani,” anasema Mafuru. Katika mashindano hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Polisi Mabatini, timu ya AR Pub ya Kilimahewa iliibuka kidedea wa mashindano hayo baada ya kuishinda Cheers Pub ya Nyakato Nundu kwa bao 1-0.

Uwanja wa CCM Kirumba ulivunja rekodi kutokana na mashabiki kujitokeza kwa mamia ambako walipata burudani iliyosheheni umahiri mkubwa wa wasanii kucheza na kulimiliki jukwaa. Miongoni mwa wasanii waliopanda jukwaani ni Ney wa Mitego, Linah, Chege, Temba, Ally Kiba, Mr Blue, Mwana FA na Young Killer ambaye alikuwa miongoni mwa wasanii wadogo nchini aliyeoneshe umahiri mkubwa katika kulimiliki jukwaa.

Wasanii wengine ni Diamond Platinum aliyekuwa kivutio kwa wakazi wa Mwanza alipopanda jukwaani kutumbuiza na kabla ya kutumbuiza aliongozana na mpenzi wake, Wema Sepetu ambapo walitembelea maeneo mbalimbali ya jiji ikiwemo ziwa Victoria. Kiukweli fiesta ya jijini Mwanza, ilikuwa ni moto wa kuotea mbali, kwani ilihudhurisha mamia ya wapenzi wa muziki wa kizazi kipya, wakiwemo vijana, watu wa makamo, kinamama na wazee.

Ney wa mitego na Nakula Vijana Ni miongoni mwa wasanii waliovutia Mwanza, Ney alikuwa miongoni mwa wasanii 20 waliohudhuria katika mkutano huo na waandishi wa habari na kisha kutumbuiza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Baadhi ya wasanii hao ni Linah, Chege, Temba, Shilole, Ally Kiba, Mr Blue, Mwana FA na Young Killer ambaye ni msanii mdogo aliyeonesha umahiri mkubwa kwa kuimba peke yake “Free style,” na Vanessa Mdee aliyekuwa kivutio cha aina yake kwa kuimba peke yake Wasanii wengine walikuwa ni Ben Pol, Christian Bella, Roma, Mkubwa na Wanawe, Barnaba, Belle 9, Rachel na Madee.

Wasanii wote walikuwa katika muonekano wa kupendeza katika mavazi ya aina mbalimbali. Ney anasema aliimba wimbo wa “Nakula Vijana,” kama njia halisi ya kuakisi maisha ya vijana wa Kitanzania ambao kwa mujibu wake, burudani ni sehemu ya maisha. “Nimeimba nakula ujana sio kwa sababu sitaki vijana wasifanye kazi, bali ni kutaka kuonesha umuhimu wa burudani baada ya kazi,” Ney alimwambia mwandishi wa makala haya.

MAZAO mengi ya chakula, matunda na biashara kama ...

foto
Mwandishi: Nashon Kennedy

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi