loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Nida yaita wananchi kuchukua vitambulisho

Ofisa wa mamlaka ya vitambulisho wilaya ya Kati Unguja, Salma Shaaban alisema baadhi ya wananchi ambao tayari wamekamilisha taratibu zote za vitambulisho hivyo, hawajajitokeza kuchukua hadi sasa.

Kwa mfano, alisema katika Shehia ya Mchangani, vitambulisho 3,000 havijachukuliwa na wahusika waliokamilisha taratibu zote.

“Tunawaomba wananchi waliokamilisha taratibu za vitambulisho vya taifa kwenda katika ofisi zetu zilizopo wilayani na kuvichukua,”alisema.

Ofisa wa operesheni ya vitambulisho vya taifa Zanzibar, Abdalla Mmanga alisema zoezi hilo linakwenda vizuri kama lilivyopangwa na wananchi wengi wamekuwa wakijitokeza kukamilisha taratibu hizo.

Aliwataka wananchi wanaofika katika vituo vya kujiandikisha vitambulisho vya taifa, kuhakikisha kwamba wanachukuwa hati zote muhimu ikiwemo cheti cha kuzaliwa na kitambulisho cha Mzanzibari mkazi.

“Zoezi la vitambulisho vya taifa linakwenda vizuri sana kwa upande wa Unguja na Pemba ambapo zaidi ya watu laki mbili wamesajiliwa,” alisema.

Zoezi la vitambulisho vya taifa linaendeshwa na NIDA kwa lengo la kusajili wananchi wote waliofikia umri wa miaka 18.

WAZIRI wa Maendeleo ya Nishati na ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi