loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Nini mbadala wa kuvunja Bunge Maalum la Katiba?

Je, Katiba Mpya inaweza kupatikana kabla ya Uchaguzi Mkuu mwakani na ikatumika katika uchaguzi huo? Swali hili, kimsingi, limeanza majibu ambayo yanaweza kuelezwa kuwa yanalingana kutoka kwa wale wanaounga mkono Mchakato wa Katiba Mpya ndani ya Bunge Maalum la Katiba na wale ambao wamesusa Bunge hilo, kwa sababu ambazo wanazijua vizuri zaidi wao wenyewe, kwa kuwa ni watu wachache nje ya kikundi hicho kidogo, wanaona mantiki ama busara ya kususa Bunge Maalum hilo.

Pande zote mbili zinaanza kukiri kuwa inawezekana usiwepo muda wa kutosha kupata Katiba Mpya kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwakani, hasa kwa kutilia maanani baadhi ya shughuli kuu zinazotakiwa kufanyika katika kipindi cha mwaka mmoja uliobakia, ukiwemo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na utayari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuendesha Uchaguzi huo pamoja na Uchaguzi Mkuu wenyewe na Kura ya Maoni ya Wananchi kuhusu Katiba Mpya.

Ni kwa sababu hizo, wale waliosusa Bunge Maalum wanasema kuwa Mchakato wa sasa wa kusaka Katiba Mpya, usimamishwe na Bunge Maalum la Katiba livunjwe ili taifa lijielekeze katika mambo mengine makubwa kama yalivyoelezwa hapo juu. Hata hivyo, msimamo huu una matatizo kadhaa. Hebu tuyaangalie.

Tatizo la kwanza la msimamo huu ni kwamba tulikubaliana tangu mwanzo kuwa sote, kama Watanzania, tunahitaji Katiba Mpya na hivyo kusimamisha Mchakato huu, unatunyima haki hii kubwa na ya msingi. Tatizo la pili ni kwamba yapo maswali kuhusu usimamishaji huo wa Bunge Maalum la Katiba na shughuli zake.

Je, tukisimamisha Mchakato wa sasa, tunausimamisha moja kwa moja na kuzika kabisa matumaini makubwa ya Watanzania? Je, utaanza tena upya? Na lini? Na chini ya uongozi na busara za kiongozi yupi? Je, tuna uhakika kuwa Rais anayekuja, atakuwa na mawazo na utayari wa Rais Kikwete kuanzisha tena mchakato huo?

Na mwisho, nani atasimamisha Bunge la Katiba, kwa sababu Rais hana madaraka hayo na sioni kama Bunge la Katiba linaweza kujisimamisha lenyewe.

Wale walioshiriki katika majadiliano ya kutunga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba walidhamiria na kukamia kikweli kweli kumwondoa kabisa ama kunyima nafasi yoyote ya maana Rais katika mchakato huu, ambalo nalo ni jambo la kuchekesha kwa kutilia maanani kuwa ni Rais ambaye alianzisha Mchakato wenyewe kwa busara zake na baada ya kushauriana na viongozi wenzake wa juu.

Kwa sababu hizo, msimamo huu unaonekana una mapungufu. Msimamo wa pili ambao umeanza kujitokeza miongoni mwa makundi ya wadau ni kwamba Mchakato huo usisimamishwe.

Badala yake uendelee, kwa kuongeza kasi, ili mahitaji yote ya Mchakato huo, kama yalivyoelekezwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Marekebisho yake, yafanyike na kukamilika, ikiwemo Kuandika Katiba Mpya na kufanyika kwa Kura ya Maoni ya Wananchi, lakini utungaji wa Sheria za kutelekeza Katiba hiyo na kuanza kutumika kwa Katiba hiyo, visubiri hadi baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwakani.

Hii ina maana kuwa Bunge Maalumu la Katiba litakuwa limekamilisha kazi yake vizuri, wananchi wamekamilisha mchango wao katika kupata Katiba Mpya kupitia Kura ya Maoni na hivyo kuliachia Bunge la Kawaida litakalochaguliwa 2015, kufanya kazi ya kutunga sheria na kanuni za kutekeleza Katiba Mpya na kuamua lini Katiba ianze kutumika.

Ikitokea kuwa Kura ya Maoni inashindwa kufikisha idadi iliyowekwa kisheria, basi zoezi hilo lirudiwe baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwakani, lakini wakati huo Katiba Mpya inakuwa tayari ikisubiri ridhaa ya wananchi.

Msimamo huo ni wa busara kwa sababu utaruhusu kukamilika kwa kazi ya Bunge Maalum la Katiba, utaruhusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwakani kufanyika bila kuingiliwa na ajenda kubwa ya Katiba na pia utawawezesha wananchi na wagombea nafasi mbali mbali katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani, kujua fika ni uwanja upi wa mapambano wanamochezea.

Msimamo wa tatu, ambao nao umejitokeza kwa nguvu sasa, unashabihiana kidogo ya ule wa pili, kwa maana kwamba Bunge Maalumu la Katiba liachiwe kumaliza kazi yake na Katiba Mpya iandikwe. Kazi isimamishwe baada ya hapo na kuachia Uchaguzi Mkuu kufanyika chini ya Katiba ya sasa.

Wenye msimamo huo wanataka kuwa Kazi ya Kupiga Kura ya Maoni ya wananchi, pamoja na utungaji wa Sheria na Kanuni za kutekeleza Katiba hiyo mpya na muda wa kuanza kutumika kwa Katiba hiyo, vifanyike baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwakani, pengine mwaka 2016 ama 2017.

Msimamo huu, kama ule wa pili, unaondoa uwezekano wa kusitishwa kwa Bunge Maalum la Katiba ambalo mpaka sasa limefanya kazi ngumu na kubwa katika kuelekea kuwapatia wananchi Katiba Mpya.

Aidha, msimamo huu, kama ule wa pili, unaleta uhakika kuwa wananchi watapata Katiba Mpya hata baada ya kustaafu kwa Rais Kikwete ambaye ameanzisha mchakato mzima wa kazi hii.

Ni misimamo hii mitatu ambayo ni dhahiri itajadiliwa katika kikao cha leo cha Rais Kikwete na wajumbe wa TCD, ambacho kama kilivyo kile cha kwanza, kinashirikisha wawakilishi wa vyama vya siasa vinavyoendelea kususia shughuli za Bunge Maalum la Katiba.

Aidha, kwa namna moja ama nyingine, mashauriano hayo ya Rais Kikwete na wajumbe wa TCD, unatoa nafasi kwa wajumbe wa kikao hicho, ambacho kama kilivyo kile cha kwanza, kinashirikisha wawakilishi wa vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni na vinavyoendelea kususa shughuli za Bunge Maalum la Katiba.

Aidha, kikao hicho pia kinahudhuriwa na mwakilishi wa vyama vya siasa visivyokuwa na uwakilishi katika Bunge la Kawaida. Aidha, kwa namna moja ama nyingine, mashauriano hayo ya Rais Kikwete na wajumbe wa TCD, yanatoa nafasi kwa wajumbe wa kile kinachoitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupata mahali pa kuficha aibu yao na kurejea Bunge Maalum la Katiba, kushirikiana na wenzao katika kusaka Katiba Mpya.

Kama ambavyo imefafanuliwa vizuri na wataalamu wa masuala ya Katiba na wananchi kwa jumla, hawa watu wachache wa UKAWA hawakuwa na sababu nyingine ya kulikimbia Bunge Maalum kwa sababu walikuwa wameshiriki katika shughuli zote za Bunge hilo kabla ya kususa na walisusa kwa sababu waliogopa wangeshindwa kura kuhusu Katiba hiyo.

Aidha, waliamini kuwa kwa watu kususa shughuli za Bunge hilo, Bunge lingekwama na kusimamisha majadiliano ya Katiba Mpya kwa Bunge kukosa sifa za kuifanya kazi hiyo.

Hili halikuwa na Bunge limeendelea na shughuli zake na linakaribia kuikamilisha kazi hiyo ya Kutunga Katiba Mpya. UKAWA wanajikosesha mchango wa kuhistoria na nafasi yao katika historia ya nchi hii. Aidha, wanajikosesha uwanja muhimu wa kisiasa.

UKAWA pia waliamini kuwa kwa kususa shughuli hiyo, Bunge Maalumu la Katiba, lisingeweza kupata asilimia stahiki ya theluthi mbili ya kupitisha Katiba Mpya kwa sehemu zote mbili za Muungano, yaani Bara na Zanzibar. Kwa hili nalo, UKAWA walijichanganya wenyewe na halieleki kuwa hivyo.

Vile vile UKAWA waliosusa Bunge wakidai kuwa wenzao katika CCM walikuwa wanawatukana sana. Lakini kwa hakika, matusi yalivurumishwa kutoka pande mbili na hata dakika ya mwisho kabla ya UKAWA kutoka Bungeni, bado waliendelea kutukana na hivyo kutoka Bungeni wakiwa wanatukana. Siyo jambo la kushangaza kwamba baada ya UKAWA kufungasha virago, matusi yameisha katika Bunge Maalum la Katiba.

Kwa sababu sasa yote ambayo UKAWA walitarajia kuyafanikisha kwa kususia Bunge Maalum la Katiba Mpya, yameshindikana na mambo hayakwenda kwa mujibu wa matarajio yao. Njia ya busara zaidi, ya ukomavu zaidi wa kisiasa na ya kuwaondolea aibu viongozi wetu ndani ya UKAWA ni kutumia nafasi ya mazungumzo ya mashauriano kati yao na Rais Kikwete, kufanya uamuzi wa busara kisiasa wa kurejea na kujiunga na wenzao katika kukamilisha kazi ya Kutunga Katiba

“WANAOFANYA shughuli za maendeleo katika vyanzo vinavyotiririsha maji ...

foto
Mwandishi: Jason Jackson Matonya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi