loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Nyalandu apiga ‘stop’ tozo za vinyago KIA

Agizo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, wakati alipokuwa Arusha kwenye soko la vinyago lililoungua mwishoni mwa mwaka jana na kuteketeza maduka 223 ya wajasiriamali wa bidhaa za vinyago vya watalii.

Nyalandu alisema tozo zilizojitokeza kwenye viwanja vya ndege, zisimame mara moja kwa sababu zinaua soko la vinyago na kukosesha mapato wajasiriamali.

“Hizi tozo zipo kinyemela, zimeanzishwa kinyemela na wanatoza mara tatu ya bei ya kinyago kilichonunuliwa, jambo linalowakera watalii kununua vinyago hivyo,” alisema.

Aidha, aliwapa mchango wajasiriamali hao mchango wa Sh milioni 100 ili kuharakisha kukamilika kwa soko hilo, ambalo lipo eneo la CCM.

“Mchango huu nataka uje mara moja na naagiza Shirika la Hifadhi za Taifa - TANAPA waandae mara moja ili pesa hii ije hapa iwasaidie hawa wajasiriamali,” alisema.

Nyalandu pia aliwataka wajasiriamali hao, wawe mabalozi wa kuitangaza TANAPA na utalii Tanzania na mabalozi wa ukarimu wa watanzania. Mwenyekiti wa soko hilo, Mgaya Ally Kondo alishukuru kwa zawadi hiyo kwa niaba ya wenzake.

Alisema wafadhili mbalimbali wamejitolea, lakini kufika hatua iliyopo sasa wanahitaji Sh milioni 130 ili kukamilisha kila kitu na wajasiriamali waanze kazi. “Lakini kwa msaada huu, tunamshukuru sana Mungu na tunaamini sasa kilio chetu kimefika mwisho.

Soko hili lina wafanyakazi zaidi ya 500, sababu kila duka kati ya 223 limeajiri wasaidizi watatu au wawili, hivyo waathirika na moto huo ni wengi,” alisema

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Arusha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi