loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Nyama kuuzwa nje ya nchi mwaka 2016

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu wakati wa kutoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) Wilaya ya Handeni.

Kikao hicho kilifanyika kufuatia ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambaye yuko mkoa wa Tanga katika kukagua utekelezaji wa Ilani na kukuimarisha chama hicho.

Muhingo alisema ili azima hiyo ifikiwe tayari uongozi umeshawaelimisha wafugaji namna ya kuzingatia ubora wa mifugo na ubora wa malisho.

“Kwa kushirikiana na Umoja wa Wafugaji Kanda ya Mashariki (UWAKAMA) tumetoa semina mbalimbali za ufugaji bora, ikiwa ni pamoja na kutembelea kituo cha utafiti wa malisho Kongwa na Ranchi ya taifa kuona umuhimu wa ufugaji bora,” alisema.

Kuhusu soko la mahindi, Muhingo alisema kutokana mavuno ya msimu uliopita kwa mzuri, wamewasiliana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Matida Burhiani ili kusaidia kuwatafutia soko wakulima wa Handeni.

Alisema miaka mwili iliyopita, wilaya hiyo ilikuwa miongoni wa wilaya zilizoomba chakula cha msaada kutokana na njaa, hali ambayo waliikataa na kuimiza kilimo cha mahindi.

Aidha, Rweyemamu alisema kwa upande wa utoro na mimba kwa wanafunzi wa kike, wamepambana nalo ikiwa ni kuwashitaki wazazi wanaokatisha wanafunzi na kuwaoza, jambo ambalo limepunguza tatizo hilo kwa kiasi kikubwa.

“Nilipofika hapa tatizo hilo lilikuwa kubwa, ulikuwa ukifika shule wanafunzi wanafikia hata kumwita mwalimu shemeji, sasa hapo patakuwa na elimu kweli?”

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi