loader
Dstv Habarileo  Mobile
Nyuma ya pazia ya wajidunga dawa za kulevya

Nyuma ya pazia ya wajidunga dawa za kulevya

Na kwamba watu milioni tatu kati ya hao wanaojidunga dawa za kulevya wamepata maambukizi ya virusi vya Ukimwi na kwamba kasi ya maambukizi ya virusi hivyo ni kubwa kwa watu wanaojidunga sindano za dawa hizo kuliko wale wanaotumia kwa njia ya kuvuta au kunusa.

Shirika la Kimataifa la Medecins du Monde (MdM), ambalo linashughulika na kutoa misaada mbalimbali ya kibinadamu ya hasa kwenye nchi na maeneo yaliyoathiriwa na magonjwa, vita, majanga ya asili, njaa na umasikini, lipo pia Tanzania ambapo husaidia jamii kwenye nyanja mbalimbali.

Akizungumzia kazi za shirika hilo nchini Ofisa Muelimishaji wa MdM, Damali Lucas anasema tatizo la matumizi ya dawa za kuleya nchini ni kubwa hivyo wameanzisha mradi wa Kupunguza Madhara kwa watumiaji wa dawa hizo. Akizungumzia hali ya matumizi ya dawa za kulevya nchini, Damali anasema bhangi ndiyo dawa za kulevya za kwanza kuanza kutumika nchini.

Pia miaka ya 1980 dawa aina ya heroini na kokaine za rangi ya kahawia zilianza kutumika nchini na baadhi ya watu ambapo mwaka 1990 matumizi ya dawa za kulevya kwa njia ya kujidunga yakaanza.

Hata hivyo mapema mwaka 2000 dawa za kulevya aina ya heroine nyeupe ikaanza kuingia nchini na watumiaji wakaendelea kuongezeka hata hivyo anasema taarifa kuhusu watumiaji wa dawa hizo ilipatikana kuwa watu takribani 200,000 nchini wanatumia dawa hizo.

Damali anabainisha kuwa taarifa ambazo sio rasmi kuhusu idadi ya watumiaji wa dawa hizo hivi sasa nchini, imeongezeka hadi kufika watu kati ya 200,000 hadi 250,000 ndio wanatumia dawa za kulevya. Inakadiriwa kuwa jijini Dar es Salaam pekee linawatumia dawa hizo kwa njia ya kujidunga 50,000 ambapo asilimia 42, ya watu hao wameambukizwa virusi vya Ukimwi.

Wakati takwimu hizo zikitoa taswira hiyo, idadi ya watu wanaoishi na virusi vya ugonjwa huo nchini ni takribani watu milioni 1.4, ya idadi ya watu milioni 44.9 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya hivi karibuni.

Methadone ni dawa mbadala inayotumika kutibu utegemezi wa vilevi na dawa kama vile heroine na Morphine ambazo hutumiwa kwa njia ya kujidunga sindano , lakini hiyo Methadone hutumika kwa kunywa kama maji na kutibu maumivu ya madhara ya dawa za kulevya.

Huduma hiyo ya Methadone ilianza kutolewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mwaka 2010 baada ya kuzinduliwa kwa miradi na programu mbalimbali za kuwasaidia watumia dawa za kulevya kuepuka au kuacha kutumia dawa hizo.

Huduma hiyo iliyoanzishwa na mtaalamu wa tiba kutoka Pangaea, Dk Douglas Bruce kwa ushirikiano na jopo la madaktari nchini na chama cha Madaktari(MAT), walianzisha huduma hiyo ambayo hadi kufika Mei mwaka jana waathirika wa dawa za kulevya 400 walikuwa wameshaanza kupatiwa huduma ya Methadone.

Hata hivyo akizungumzia hali ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa watumia dawa za kulevya katika Wilaya ya Temeke, Damali anasema MdM kupitia mradi wa Kupunguza Madhara kwa Watumia Dawa za Kulevya, walifanya utafiti kwenye wilaya hiyo ambapo watumiaji 430 wa dawa hizo walihojiwa.

Watumiaji hao, 357 ni wanaume na 73 ni wanawake na kwamba 267 wanatumia dawa za kulevya kwa njia ya kujidunga sindano na 167 wanatumia kwa njia ya kuvuta na kunusa. Hata hivyo baada ya kuhojiwa na kuelimishwa madhara ya matumizi ya dawa hizo, baadhi yao walikubali kupima virusi vya Ukimwi ambapo asilimia 26 ya waliokubali kupima walionekana kuwa na maambukizi ya virusi hivyo.

Akifafanua anasema wengi wa waliobainika kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi ni wale wanaojidunga dawa hizo ambapo ni asilimia 34.8 ya asilimia hiyo 26 na wale wanaotumia kwa kunusa na kuvuta waliokuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi ni asilimia 11.7 Hata hivyo asilimia 18 ya watumiaji waliokubali kupima walionekana kuwa na maambukizi ya homa ya ini na hao ni wale wanaotumia dawa za kulevya kwa njia ya kujidunga.

Anasema utafiti wao unaonesha kuwa kwa Wilaya ya Temeke pekee maambukizi ya virusi vya Ukimwi hasa kwa watumia dawa za kulevya ni makubwa kwa kuwa wengi wao hushirikiana mabomba ya sindano na kama mmoja wao anavirusi hivyo ni rahisi kusambaza kwa wengine.

“tumefanya uchunguzi tumegundua kuwa bomba moja la sindano linatumika kwa watu zaidi ya mmoja kwa siku nne, na hiyo ni hatari, wengi wao wanaambukizana kwa kutofahamu, tuwasaidie hawa wasiendelee kuambukizana”, anasema Damali. Akizungumzia hali ya tatizo la dawa za kulevya lilivyo, Saidi Selemani (28), mkazi wa Mtongani Dar es Salaam alianza kutumia dawa za kulevya kutokana na kujiingiza kwenye makundi ya vijana yasiyofaa.

“Nilikuwa mcheza show, nilipata hela siku moja katika mizunguko yangu nilikutana na rafiki yangu wa zamani katika maongezi yetu kumbe yeye alikuwa anatumia dawa nilijikuta naingia huko”, anasema Selemani. Hata hivyo anaendelea kusema baada ya muda alikimbiwa na mzazi mwenzake na hali ya maisha ikawa mbaya na baada ya kupewa elimu na kuambiwa madhara ya dawa hizo, anatamani sasa kupunguza dozi.

“Niko katika harakati za kuacha, nahitaji kupunguza dozi nitaacha kutumia hizo dawa, kwa muda wote niliotumia tangu mwaka 1999 nikiwa darasa la sita zijaona faida,nimerudi nyuma kimaisha, nitaanza kutumia Methadone ili inisaidie kuondoka kwenye hatari iliyo mbele yangu”, anamalizia Selemani. Vita dhidi ya dawa za kulevya ni ya jamii yote, tuwasaidie watumiaji wa dawa hizo wapunguze madhara yakiwemo maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

OFISI ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) ni Taasisi ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi