loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Ofisi ya CAG yaendelea kukusanya vielelezo IPTL

Taarifa iliyotolewa jana na NAO kupitia kwa msemaji wake Sarah Reuben, ilieleza kuwa ukusanyaji huo wa maelezo yanayoendana na vielelezo vinavyohitajika ni muhimu ili kumsaidia mkaguzi kufikia malengo ya ukaguzi huo ambao umeagizwa kufanywa na ofisi ya Katibu wa Bunge na Ofisi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.

"Ukusanyaji wa taarifa hizo unategemea wahusika kutoka taasisi za Serikali, mashirika ya umma na taasisi na watu binafsi waliopo nchini na nje ya nchi ambao ni wadau katika suala hili," ilisema taarifa hiyo.

Ukaguzi huu unalenga kufanya uchunguzi wa kina ambao utatoa taarifa kamili yenye kuonesha hali halisi kuhusu miamala kwenye akaunti maalumu ya Tegeta Escrow kisha kutoa taarifa kuhusiana na ukaguzi huo.

Ukaguzi unaofanywa ni kuhusu madai ya kuchotwa kwa Sh bilioni 201 za akaunti ya Teeta Escrow na mazingira ya kuchukuliwa kwake.

Fedha hizo ziliwekwa katika akaunti hiyo na wadau, Tanesco na IPTL baada ya kuibuka mgogoro wa kisheria kutokana na madai kuwa shirika hilo la umeme lilikuwa linalipa gharama kubwa za uwekezaji zaidi ya makubaliano.

Iliamriwa fedha hizo zihifadhiwe hadi mgogoro utakapokwisha, lakini fedha hizo zikachukuliwa na kampuni iliyonunua IPTL, Pan African Power Solution (PAP) jambo ambalo limekuwa linalalamikiwa na baadhi ya wabunge kuwa uchotaji wa fedha hizo ni wizi mkubwa ambao umefanywa na baadhi ya vigogo serikalini.

Hata hivyo, taarifa hiyo ilifafanua kuwa licha ya changamoto zilizoainishwa, ukaguzi wa IPTL unaendelea na muelekeo ni mzuri kwa sababu ni maeneo machache tu yaliyobaki ambapo yatakapokamilika ofisi hiyo itawasilisha ripoti kwa taasisi zilizouomba ukaguzi huo kwa mujibu wa Sheria.

Pia ofisi hiyo imeeleza kuridhishwa na ushirikiano mzuri inaoendelea kuupata kutoka kwa wadau wa ukaguzi huo. Kutokana na ukaguzi huo kuendelea kufanywa, NAO imesema itakuwa ni kinyume na utaratibu kuzungumzia kwa kina taarifa ya ukaguzi wa IPTL kwa sasa.

WAZIRI wa Maendeleo ya Nishati na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi