loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Okwi aiumiza kichwa Yanga

Juzi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Kamati yake ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji, lilitangaza kuzuia mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda hadi itakapopata ufafanuzi kutoka Fifa, Akizungumza na gazeti hili, Katibu Mkuu wa Yanga, Bernard Njovu alisema Yanga ina utaratibu wa kushirikiana na Kamati yake ya Usajili katika kila jambo kuhusu masuala ya usajili.

Njovu alisema katika suala la Okwi, kila kitu kilikuwa sawa na ndio maana Kamati ya Utendaji iliridhia mchezaji huyo kutua kwa mabingwa hao wa Tanzania Bara. Alisema wamesikia taarifa kuzuiwa mchezaji huyo kucheza kwa mshangao mkubwa na kuongeza kuwa hata hivyo hawajapewa taarifa maalumu.

“Sisi tumesikia hili katika vyombo vya habari, hivyo hadi leo (jana) hatukuwa na taarifa rasmi kutoka kwa TFF kutueleza kuzuiliwa kwa mchezaji huyu,” alieleza Njovu.

Hata hivyo, alisema wanawasiliana na TFF ili kupatiwa taarifa hiyo ili kujua ni nini hasa kinachotakiwa. Alisema barua hiyo itatoa taarifa halisi kuhusu kinachotakiwa kufanywa kwa sasa na klabu hiyo.

Katika taarifa yake hiyo kwa vyombo vya habari, TFF ilisisitiza kuwa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imebaini kuwa Okwi aliruhusiwa kuichezea SC Villa ya Uganda kwa kibali maalumu kutoka Fifa.

Kamati hiyo ilibaini kuwa Okwi aliyekuwa na mgogoro na klabu yake ya Etoile du Sahel aliruhusiwa na Fifa kuchezea SC Villa kwa kibali maalumu cha miezi sita ili kulinda kiwango chake wakati suala lake dhidi ya Etoile du Sahel likishughulikiwa na shirikisho hilo la kimataifa.

Kutokana na hali hiyo, TFF iliamua kumzuia kwanza kuendelea kuichezea Yanga na kuandika barua kwenda Fifa yenye kutaka kufahamu iwapo mchezaji huyo anaweza kucheza ligi Tanzania wakati Etoile du Sahel ikiwa imefungua kesi katika shirikisho hilo la kimataifa ikidai Okwi bado ni mchezaji wake.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage aliwaambia waandishi wa habari kuwa amepata barua kutoka kwa Mmwanasheria wa Fifa ikiitaka Etoile kuijibu Simba ifikapo Jumatatu ijayo. Rage alisema ikiwa haitafanya hivyo majibu yatatolewa Januari 28 na Fifa kwamba ni kitu gani kinafuata.

“Tunasubiri majibu ya barua hiyo ikiwa yatafanyiwa kazi basi ujue Simba itapata baraka, kilichobaki tunamwachia Mwenyezi Mungu,” alisema Rage. Mpaka sasa, Fifa kuna kesi tatu kuhusu Okwi.

Wakati Okwi ameishtaki klabu hiyo kwa kutomlipa mshahara, Etoile du Sahel imemshitaki mchezaji huyo kwa utoro. Nayo Simba imeishtaki Etoile du Sahel kwa kushindwa kuilipa ada ya mauzo ya mchezaji huyo ambayo ni Dola za Marekani 300,000.

Kuhusu suala la Shomari Kapombe kushindwa kurudi Ufaransa kwa madai ya kutolipwa msharahara katika klabu ya AS Canes, Rage alisema alifuatilia na kuzungumza na Mkurugenzi wa klabu hiyo ili kujua tatizo na kudaiwa ni kweli hakulipwa mshahara wa Novemba mwaka jana.

Alisema klabu hiyo bado inamhitaji Kapombe na iko tayari kumlipa mshahara huo ikiwa itahakikishwa kuwa anarudi kuichezea klabu hiyo.

“Jana nilipata ujumbe kwenye mtandao kutoka kwa Mkurugenzi wa Kapombe ukieleza kuwa Kapombe hakulipwa mshahara wa Novemba, akasema Kapombe tunamthamini isipokuwa anatusumbua, arudi na sisi tuko tayari kumlipa,” alisema Rage.

Rage alifafanua kuwa Kapombe ana mkataba na AS Canes wa miaka miwili na pia Simba hadi 2016, hivyo alikuwa akishangazwa na baadhi ya taarifa zinazoonesha kuwa baadhi ya klabu zilikuwa zikitaka kumsajili bila kuwasiliana na wakala wake aliyeko Uholanzi.

Alisema hapendi kuona Kapombe anarudi nyuma na zaidi kuona mafanikio yake ili kuleta heshima katika nchi kwani atakapouzwa katika timu za Ulaya, mapato yake yatakuwa ni makubwa.

Aliwahimiza wachezaji wa Tanzania wanapopata nafasi, wasikimbilie kucheza Simba na Yanga peke yake, wabadilike kuendana na wakati.

KLABU ya Simba  imetambulisha  mashindano mapya ya Super  Cup, ...

foto
Mwandishi: Waandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi