loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Okwi azuiwa Yanga

Kwa mujibu wa taarifa ya TFF iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao cha Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana jana kupitia masuala mbalimbali.

Taarifa hiyo ilisema, Kamati hiyo imeamua kusimamisha usajili wa Okwi Yanga baada ya kubaini kuwa mchezaji huyo aliruhusiwa kuichezea SC Villa ya Uganda kwa kibali maalumu kutoka FIFA.

Okwi ambaye aliingia mgogoro na klabu yake ya Etoile du Sahel ya Tunisia aliruhusiwa na FIFA kuchezea SC Villa kwa kibali maalumu (provisional permit) cha miezi sita ili kulinda kiwango chake wakati suala lake dhidi ya Etoile du Sahel likishughulikiwa na shirikisho hilo la kimataifa. Mpaka sasa FIFA kuna kesi tatu kuhusiana na suala la mchezaji huyo.

Wakati Okwi ameishitaki klabu hiyo FIFA kwa kutomlipa mshahara, Etoile du Sahel imemshitaki mchezaji huyo kwa utoro. Nayo Simba imeishitaki Etoile du Sahel kwa kushindwa kuilipa ada ya mauzo ya mchezaji huyo ambayo ni dola za Marekani 300,000.

“Hivyo, TFF imeiandikia FIFA kutaka kujua iwapo mchezaji huyo anaweza kucheza Ligi nchini Tanzania wakati Etoile du Sahel ikiwa imefungua kesi katika shirikisho hilo la kimataifa ikidai Okwi bado ni mchezaji wake,” ilisema taarifa hiyo.

Okwi aliyekuwa akichezea Simba, aliuzwa kwa Etoile mwanzoni mwa mwaka jana, lakini usajili wake kwa klabu hiyo ya Tunisia haukuwa mzuri kwa upande wake baada ya kukosa namba.

Aidha, Simba mara kadhaa ilikuwa ikiilalamikia Etoile kwa kutowalipa fedha walizomuuza mchezaji huyo hali iliyosababisha kushitaki FIFA, ambapo pia ilishatuma fedha kuwezesha shauri lao kusikilizwa lakini mpaka sasa FIFA bado haijatoa kauli yoyote kuhusiana na hilo.

Okwi yupo na Yanga Uturuki walipokwenda kwa kambi ya mazoezi ya wiki mbili na wanatarajia kurejea nchini kesho kabla ya kuanza kurusha kete yake dhidi ya Ashanti United katika mechi ya kwanza ya mzunguko wa pili keshokutwa.

Klabu ya Liverpool na Manchester United zipo vitani kumuwinda ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi