loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Olympiakos yaionya Manchester United

Michel anatarajia kupata changamoto kubwa, na Mhispania huyo amemtaka David Moyes ajiandae vya kutosha.

Michel alisema: "Mwanzoni mwa msimu nilisema kwamba kushinda ligi na kombe la ligi ni changamoto, kushindana Ulaya ni kitu kingine kabisa".

"Benfica, Anderlecht, PSG, sasa United, hapa na Old Trafford. Niliwaambia wachezaji wangu kwamba mechi hii ni maalumu na ya kipekee kabisa".

"Tunajua na wao watafanya kila wanaloweza kushinda, lakini nasi tuna mipango yetu kuhusu mechi hii". Alisema, Olympiakos kukutana na mashetani hao wekundu kunafanya mechi hiyo kuwa ya kipekee.

"Hatutazuia, tutazuia na kufanya mashambulizi pia, tunataka kushinda mechi hiyo, tunataka kufunga mabao," alisema.

Kutofanya vizuri kwa United kwenye kutetea ligi huenda kukawa sababu ya Olympiakos kutamba kushinda mechi hiyo.

"Tunataka kufurahia mashindano ya Ulaya, lakini nani anasema kwamba hatuwezi? Nani anasema kwamba hatuko tayari kushindana na United, tutashindana nao".

Mechi nyingine itakayochezwa leo Zenit St Petersburg na Borussia Dortmund.

VINARA wa Ligi Kuu soka Tanzania, Azam FC ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi