loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Oman, Zanzibar kuimarisha uhusiano

Hayo yalisemwa na Balozi mdogo wa Oman nchini, Saleh Al-Hafidh wakati alipozungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad ofisini kwake alikokwenda kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.

Alisema uhusiano wa Oman na Zanzibar, umeimarika zaidi katika kipindi cha miaka kumi ambapo nchi mbili hizo zimefikia makubaliano mbali mbali yenye lengo la kuleta maendeleo na kuimarisha uchumi.

Alitoa mfano kwamba makubaliano yaliyofikiwa na nchi mbili hizo na kutoa nafasi zaidi za masomo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa Zanzibar ni changamoto kubwa ya kupata wataalamu katika sekta mbali mbali.

“Serikali ya Oman ipo tayari kusaidia maendeleo ya Zanzibar katika sekta mbali mbali ikiwemo afya na elimu ya juu...Sekta hizo mchango wake katika ukuaji wa uchumi ni mkubwa sana,” alisema.

Alitoa mfano kwamba Oman imekuwa mstari wa mbele, kusaidia maendeleo ya sekta ya afya kwa kuimarisha Chuo cha Afya kilichoko Mbweni, ambacho sasa ni sehemu ya Chuo kikuu cha Zanzibar.

Aidha, alisema kufanyika kwa tamasha la kiislamu hivi karibuni Zanzibar kwa kiasi kikubwa, limesaidia kuitangaza Zanzibar katika sekta ya utalii kwa nchi za Kiarabu kuleta wageni wengi zaidi Zanzibar. Mapema, Maalim Seif alisifu uhusiano wa Zanzibar na Oman na kusema ni wa kindugu wenye historia kubwa.

Alipongeza Serikali ya Oman kwa misaada yake katika sekta mbali mbali, ambayo imelenga katika kupiga hatua kubwa ya maendeleo kwa kuimarisha sekta za elimu na afya.

Hivi karibuni, Serikali ya Oman na Zanzibar imekubali kuwapatia nafasi za juu wanafunzi wa Zanzibar, kusoma katika vyuo vikuu mbali mbali duniani, ikiwa ni ufadhili wa masomo kutoka kwa Sultani Qaboos.

Aidha, Serikali ya Oman imekubali kusaidia na kuimarisha masuala ya nyaraka mbalimbali na majengo ya kale ya makumbusho kwa ajili ya kulinda na kutunza historia katika kukuza sekta ya utalii.

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi