loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ondokeni sehemu za watembea kwa miguu yasema DART

Dart ametaka wafanyabiashara hao kwenda kwenye maeneo ambayo serikali imetenga badala ya kuvamia maeneo yaliyojengwa kwa ajili ya mabasi yaendayo haraka.

Hatua hiyo imekuja baada ya timu ya maofisa kutoka kwa Wakala kufanya ukaguzi kuangalia maendeleo ya mradi huo ambao kwa sasa upo katika hatua za mwisho kabla ya mkandarasi kuukabili rasmi kwa serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la Kimara jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Usafirishaji na Mipango wa DART Serapion Tigahwa, alisema ni vyema wananchi na wafanyabiashara wakatambua kuwa serikali haimkatazi mtu kufanya biashara, lakini yapo maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli hizo.

Alisema imebaki miezi michache kwa ajili ya mradi huo kukabidhiwa na kuanza kufanya kazi. Alisema ni jambo la aibu kuanza kuharibu miundombinu na kufanya kazi kinyume na matarajio yaliyokusudiwa.

“Barabara hizi zimejengwa kwa ajili ya mabasi yaendayo haraka na si vinginevyo,” alisisitiza Tigahwa na kuongeza kuwa maeneo yaliyojengwa kwa ajili ya watembea kwa miguu yamegeuzwa sehemu za kuegesha pikipiki. “Hatuwezi kuvumilia hali hii ya uharibifu na matumizi hovyo ya miundombinu kwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakayekiuka maagizo hayo na kuendelea kubaki katika maeneo ya mradi basi hatua kali zitachukuliwa,” alisema.

Mshauri Mkuu wa Ufundi wa Dart, Dieter Schelling ambaye alikuwepo kwenye ziara hiyo ya kukagua maendeleo ya mradi, alisema jitihada za makusudi lazima zifanywe kulinda miundombinu ya maradi.

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi