loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pinda ataka maslahi ya wananchi mikataba ya madini

Alitoa mwito huo jana wakati akifungua semina ya siku tano juu ya mafunzo ya kuingia makubaliano na mikataba kwenye sekta ya madini kwa wanasheria wa sekta ya umma kutoka nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.

Katika mkutano huo ulioanza jana jijini Dar es Salaam, Pinda alisema wanasheria wanapaswa kujali wananchi walio masikini kwa sababu wao hawana fursa ya kuingia kwenye vikao kama vyao na kutoa sauti juu ya kile wanachokitaka.

“Licha ya umasi kini wao, wanaishi juu ya ardhi ambayo chini yake kuna utajiri tele wa madini na rasilimali nyingine. Ninawasihi sana muwafikirie watu hawa kabla ya kufanya uamuzi wowote,” alisisitiza.

Alisema ili jambo hilo liweze kufanikiwa ni lazima, wanasheria kama wadau wa mwanzo kabisa, wakubali kukataa kupokea fedha chafu na vishawishi kutoka kwa wawekezaji na siku zote waweke uzalendo mbele kwa maslahi ya nchi zao.

Alisema rasilimali za a Afrika hazijaleta maendeleo kwa wakazi wake kwa sababu wanaofaidika ni kampuni kubwa kutoka nje na watu wachache wenye nafasi huku walio wengi wakiambulia patupu.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, ni theluthi moja ya mikataba ya uchimbaji madini inayofaidisha bara zima la Afrika ikilinganishwa na faida ambayo bara la Amerika Kusini inanufaika nalo.

Ili kuepukana na hali hiyo, Waziri Mkuu alisema umefika wakati wa kukataa kutoa misamaha ya kodi kwa kampuni za kimataifa na kuhakikisha zinalipa kodi katika kila nchi husika ya Afrika Mashariki.

Alisema umefika wakati wa kuhakikisha Serikali za nchi husika zinaweka sera madhubuti na miongozo ya kisheria itakayohakikisha mikataba inayoandaliwa kwa ajili ya utafutaji na uendelezaji wa madini na rasilimali zake inazinufaisha nchi kwanza.

Akimkaribisha Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema sekta ya madini ni mojawapo ya sekta zinazokua kwa haraka nchini lakini inachangia chini ya asilimia moja ya ajira zote nchini. Washiriki wa mkutano huo ni kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Tanzania.

MCHICHA ni aina nyingine za ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi