loader
Picha

Pinda mgeni rasmi Tamasha la Mtwara

Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti Mtendaji wa Tacin ambayo inaandaa tamasha hilo, Anic Kashasha alisema maandalizi yanaendelea vema hadi sasa.

Alisema tamasha hilo litashirikisha pia washiriki na wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara, lengo kuu likiwa ni kuwapatia fursa ya kufahamu masuala mengi yahusuyo sanaa, uchumi na fursa za kimaendeleo.

Alisema kuwa mbali na burudani, pia kutakuwa na Idara, Taasisi za Serikali pamoja na wadau wengine mbalimbali wa shughuli za kimaendeleo.

Alisema kuwa wadau wa kilimo, uvuvi, ufugaji, utalii na wengine watajumuika katika kuwapatia vijana elimu kuhusu sekta hiyo.

Alisema katika tamasha hilo, wananchi wa mikoa hiyo watajumuika pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo na kujifunza mengi katika nyanja hizo.

“Mtwara Festival, ambao ni mpango mkakati wa mawasiliano wa kuhamasisha wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi, kizitambua fursa shirikishi zinazosisimuliwa na uchumi wa gesi asilia,” alisema Anic.

BAADHI ya makocha na wachambuzi wa soka nchini ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi