loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pombe inavyoweza kuwa chanzo cha ukatili wa kijinsia

Wote wanaamka kumlaki baba yao ambaye akili na busara vimekwenda likizo. Hii ni mikasa inayowakumba wanawake wengi ambao hulazimika kuvumilia tabia za wazazi wenzao kutokana na ulevi na mambo yote yanayoambatana na unywaji wa pombe kupita kiasi.

Wanaume hawa hurudi makwao usiku wa manane na kuwasumbua wake zao. Wakati mwingine hudai chakula ambacho hawakuacha fedha ya matumizi wakati wakiondoka.

Lakini jambo lingine ambalo ni baya zaidi ni pale mwanamume huyo anapoamua kurudi nyumbani na hasira za bandia na kutembeza kipigo kwa mke na watoto bila sababu za msingi.

Kipigo hiki huambatana na matusi pamoja na maonyo kadhaa pale mwanamke anapothubutu kutamka kwamba atafikisha mambo hayo kwa wazee au vyombo vya sheria. Ulevi huchangia kudumaa kwa uchumi wa familia.

Mzazi hasa wa kiume anaweza kutumia mshahara wote na mtaji wa biashara kwenye ulevi. Tena ulevi huo haufanyi peke yake bali na rafiki zake wa pombe ambao asubuhi huwa hawana msaada wowote pale wanapobaini kuwa rafiki yao ametumia fedha yote kwenye pombe na hata hela ya supu hana.

Ulevi ni chanzo cha mateso na migogoro mingi ya kifamilia . Wakati mwingine husababisha mahusiano ya ndoa kuvunjika pale uvumilivu unapofikia kikomo. Ulevi siyo kisingizio cha kusababisha tabu kwenye familia .

Hii inatokana na maonyo mbalimbali ambayo yanatolewa hata na kampuni zinazouza vilevi. Unywaji wa pombe chini ya miaka 18 umekatazwa.

Aidha, yapo maonyo ya athari za ulevi kwa afya ya binadamu na pia pombe ikizidi humfanya mtu kutumia akili ya kuazima na hivyo kudidimiza maendeleo ya familia. Hali ya ulevi kwa wanaume huwa mbaya zaidi pale ambapo mwanamke ni tegemezi. Maana fedha ambayo mwanamume hupata huweza kuishia kwenye ulevi na familia ikakosa mambo ya msingi kama chakula na nguo.

Mwanamke anaweza pia kutokuwa mzalishaji kiuchumi kutokana na kipigo cha kilevi kutoka kwa mwenzake. Sote tunafahamu mchango wa vileo kwenye pato la taifa kwa njia ya kodi.

Tunafahamu burudani ya pombe pale inapotumika kwa ustaarabu katika sherehe na matukio mengine.

Lakini pombe inapozidi kipimo ni janga kwa jamii. Waandishi wa habari wana mchango wa kipekee kuelimisha jamii juu ya matumizi sahihi ya vileo na athari za tabia za kilevi. Semina na mafunzo mbalimbali yanapotolewa na wadau mbalimbali kama TAMWA, Wizara ya Afya na viongozi wa dini yatiliwe manaani vya kutosha ili kuwalinda wanawake kutokana na ukatili wa kijinsia unaoweza kufanywa kwa sababu za ulevi.

Ni vema jamii ikachukua hatua za msingi kuendelea kuwaonya wanafamilia juu ya mambo ya maendeleo. Kwa maelezo ya kina, Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kinafanya juhudi za ziada kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya kuitangaza nchi yetu katika masuala ua ukatili wa kijinsia.

Moja ya mambo ambayo TAMWA huyapa kipaumbele cha kipekee ni masuala ya kuepuka tabia za kilevi ambazo zinachochea ukatili wa kijinsia.

TAMWA inajihusisha na utafiti na kutoa machapisho mbalimbali ambayo kwa miaka mingi wamewasaidia wananchi na Serikali kutambua na kufahamu hatua stahiki juu ya kupambana na ukatili huu.

Ni vema sasa jamii ikafahamu kwamba wapo wadau ambao wanalia pamoja na waathirika wa ukatili wa kijinsia.

Ni vema sasa wananchi wakaamua kwa dhati kabisa kuelimishana juu ya masuala ya matumizi mazuri ya vileo ili kujenga taifa la wanaume na wanawake wenye busara kwa ustawi wa jamii. ntayombaa@yahoo.com

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya ...

foto
Mwandishi: Alpha Ntayomba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi