loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Prof. Kamuzora ateuliwa bodi ya kimataifa ya CTA

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa CTA, Michael Hailu, uteuzi huo ni wa miaka mitano kuanzia Novemba 7, 2013 hadi Novemba 6, 2018. Prof. Kamuzora pia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe anayeshughulikia Utawala na Fedha.

Bodi ya CTA inaundwa na wajumbe sita, watatu kutoka Afrika, Karibiani na Pasifiki na watatu wengine kutoka Umoja wa Ulaya. Prof. Kamuzora atawakilisha ukanda wa mashariki wa Afrika katika bodi hiyo.

Mkurugenzi wa Mawasiliano, Chuo Kikuu Mzumbe, Rainfrida Ngatunga alisema katika taarifa yake jana kuwa uteuzi wa Prof. Kamuzora ni sifa kwa chuo hicho, Tanzania na Afrika kwa ujumla.

“Tunampongeza kwa uteuzi wake…hii imeiletea sifa Mzumbe na kuifanya Tanzania ing’are katika anga za kimataifa zaidi,” alisema katika taarifa yake.

Ngatunga alimwelezea Prof. Kamuzora kuwa ni mchapakazi mwenye uzoefu wa kutosha na ndiyo maana anapata mafanikio makubwa.

CTA yenye makao makuu yake Wageningen, Uholanzi, ni moja ya taasisi zilizoundwa ili kutekeleza makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki kwa upande mmoja na nchi za Umoja wa Ulaya kwa upande mwingine.

Mkataba huo ulisainiwa Cotonou Juni 23, 2000 na kurekebishwa tena Juni 25, 2005, Luxembourg na Juni 22, 2010, Ouagadougou. CTA inalenga kuimarisha sera na kujenga uwezo wa taasisi wa nchi za ACP, zinazojihusisha na kilimo na maendeleo vijijini.

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amemteua Lucas ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi