loader
Dstv Habarileo  Mobile
Punda: Mnyama mwenye uwezo wa kufanya maamuzi

Punda: Mnyama mwenye uwezo wa kufanya maamuzi

Punda wanapatikana sehemu mbalimbali duniani na asili yao ni punda mwitu ambaye asili yake ni Afrika hasa sehemu za jangwani. Punda ni mnyama mkubwa kuliko pundamilia na ana nguvu kuliko farasi wenye kimo sawa na yeye. Wana macho makubwa kuliko wanyama wote wa nchi kavu, na wanasifika katika kazi ya usafirishaji wa watu na mizigo.

Pia wanatumika kwa kazi za mashambani, kuvuta magari na mashine mbalimbali. Kuna aina tatu za punda ambazo ni ni punda wenye asili ya Ulaya na Tarpani ambao wametoweka. Aina ya pili ni punda wanaofugwa na aina ya tatu ni punda mwitu ambao wako katika hatari ya kutoweka. Punda wana rangi ya kahawia, nyeusi na nyeupe.

Pia kuna punda wenye rangi mchanganyiko na hutofautiana kimo kulingana na mazingira wanayoishi. Punda wakubwa zaidi wana uzito wa kilogramu 1,000 na hutumiwa kwa kazi nzito za mashambani au msituni kama vile kuvuta magogo. Punda wako kwenye kundi la wanyama wanaokula majani.

Wana uwezo wa kula nyasi kilo saba hadi 11 za majani kila siku na kunywa maji lita 38 hadi 45 kwa siku. Mtaalamu wa afya ya punda na farasi, David Hadrill anasema punda wadogo huwa na meno 38 na wanapokomaa huota meno manne ya ziada na kuwafanya kuwa na jumla ya meno 42.

Ana uwezo wa kuonja chakula chake kama ni kitamu au la. Hivyo akipewa majani matamu hula kwa wingi ila akipewa majani machungu au yanayoweza kumdhuru hukataa kula. Mfumo wa tumbo la punda haumwezeshi kutapika hivyo huwa makini anapokula chakula kwa kuwa hawezi kutapika chakula kinachomdhuru. Pia hana uwezo wa kupumua kwa mdomo.

Tafiti mbalimbali kuhusu punda zinaeleza kuwa ilianza kufugwa katika bara la Asia miaka 3000 kabla ya Kristo na kisha kuenea sehemu mbalimbali duniani. Baadhi ya watu hufuga punda kwa ajili ya maziwa na nyama. Pia wapo wanaofuga wanyama hao kwa lengo la kuwatumikisha katika kazi hasa kubeba mizigo, kuvuta magari na mikokoteni na kupeleka watoto shule.

Wapo wanaotumia punda kama kibanda cha kuuzia magazeti, punda kutumika pia kama maktaba ya mtaa ambapo huvishwa nguo yenye mifuko inayotumika kuhifadhi vitabu.

Punda anayetumika kama maktaba husimama karibu na vituo vya mabasi, katika mlango wa kuingia shule na kwenye maeneo ya wazi ili watu waweze kuchukua na kusoma vitabu na magazeti wakati wanaposubiri usafiri au kuwa katika mapumziko mafupi kwenye sehemu za wazi.

Punda wa mwituni wanaishi katika makundi kulingana na kaliba yao. Wanaweza kukusanyika kwenye makundi kulingana na aina ya punda pia huweza kuishi na wanyama wengine kama mbuzi bila matatizo. Punda wana uwezo wa kulala usingizi wakiwa wamesimama wima. Miguu yao huwawezesha kulala pasipo kuanguka. Hata hivyo hulala usingizi mnono wanapokuwa wamejilaza chini.

Mfumo wao wa kulala huwawezesha punda mwitu kuwekeana zamu ya kulinda kundi hivyo baadhi ya punda kulala usingizi wa mang’amung’amu wakiwa wamesimama huku wengine wakiwa wamejilaza chini na kupata usingizi mzito. Kwa kawaida hulala wastani wa saa tatu hadi nne kwa siku.

Punda wanaona vizuri ingawa hawawezi kutambua vyema rangi nyekundu na nyingine zinazoshabihiana na nyekundu. Wana uwezo wa kuzungusha masikio yao kwa nyuzi 180 hivyo husikia vizuri bila kugeuza shingo. Uwezo wao wa kusikia, kuona na kuhisi ni mkubwa kuliko binadamu.

Ingawa watu wengi hudharau punda, inaelezwa ni miongoni mwa wanyama wenye akili nyingi na wana uwezo wa kufanya maamuzi na kushikilia msimamo kiasi kwamba binadamu hawezi kumlazimisha kubadili maamuzi hayo. Kwa kuwa uwezo wao wa kuona kusikia na kuhisi ni mkubwa hutumia akili kupima kila jambo ili kujiepusha na hatari.

Wanapobaini jambo la hatari hukaidi kufanya kitu wanachoamrishwa na binadamu. Msimamo wao katika kufanya maamuzi ndio uliosababisha msemo wa wahenga kuwa unaweza kumlazimisha punda kwenda kisimani lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji. Watu wenye utaalamu wa kufanya mawasiliano na punda huweza kuepuka hatari kwa kusoma mwenendo wa punda katika vita au katika safari za kawaida.

Punda wana uwezo wa kutambua au kuhesabu vitu visivyozidi vitatu, wana uwezo wa kufikiri na kutafakari hasa wanapokutana na kitu kisicho cha kawaida. Akiona kiti kisichokuwa cha kawaida husimama kwa muda kama mtu anayetafakari jambo kwa makini na kama akiridhika anaweza kuendelea na safari, kubadili njia au kurudi alipotoka na hufanya hivyo bila kuongozwa na mtu. Punda ana kumbukumbu nzuri na uwezo wa kutambua sehemu alizoishi au kupita.

Endapo utamhamisha eneo na kumpeleka mbali ambapo atakaa kwa zaidi ya miaka 20 siku akirudi anatambua njia na kwenda moja kwa moja katika banda lake la zamani. Inaelezwa kuwa punda jike wana mahaba na sio wasumbufu wakati wanapofuatwa na dume. Hata hivyo dume ndio wenye maringo zaidi kwa kuwa huchagua majike yenye nguvu ili waweze kupata watoto wazuri na wenye maumbo wakubwa.

Punda hubeba mimba kwa kipindi cha miezi 11 ila kuna wanaochukua muda mrefu zaidi hadi mwaka mmoja na juma moja. Kwa kawaida wanazaa ndama mmoja na ni nadra kuzaa mapacha. Ndama wa punda anaweza kusimama na kukimbiakimbia muda mfupi baada ya kuzaliwa. Punda huzaa wakati wa masika na hunyonyeshwa kati ya miezi minne hadi sita.

Punda huanza kufundishwa kazi akiwa na umri wa miaka miwili hadi minne. Punda hasa dume hukomaa na kuanza kupanda jike akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu ila mifupa yake huendelea kukua na kukomaa hadi anapofika umri wa miaka sita. Hata hivyo, umri wa kuzaliana hutofautiana kati ya punda mwitu na punda wa kufugwa ambao uhuru wao wa kujamiiana ni mdogo ikilinganishwa na punda mwitu.

Uwezo wa punda kujamiiana unatofautiana kwa umri kutokana na aina ya punda, ubora wa matunzo, na mazingira. Punda wanaopewa matunzo mazuri na wenye eneo kubwa la kuishi huanza kujamiiana mapema ikilinganishwa na punda wasiokuwa na matunzo mazuri au wanaoishi sehemu ndogo.

Pia punda huanza mafunzo ya kazi wakiwa na umri tofauti kulingana na kazi husika. Punda wa kazi za nyumbani kama vile kubeba mizigo na watu, huanza kufundishwa kazi wakiwa na umri wa miaka miwili hadi mitatu.

Punda ni miongoni mwa wanyama wasiopenda upweke. Punda anayefugwa akiwa peke yake husogea na kuchanganyika na watu pia huweza kukaa karibu na mbuzi au kondoo. Punda anayetengwa au kuwekwa peke yake huwa na hasira kwa kuwa hawapendi hali ya upweke. Makala haya yameandaliwa kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya habari.

Mteja anayetaka kutuma mzigo nje au kupitishia ...

foto
Mwandishi: Kaanaeli Kaale

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi