loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rage: Malinzi hapana, Wambura arejea TFF

Rage aliwaambia waandishi wa habari hapa jana kuwa amemwandikia barua Malinzi akimwomba kufikiria upya uamuzi wake kwa sababu hatua hiyo ina athari mbaya kwa Simba na nchi kwa ujumla.

Jumapili iliyopita, Malinzi alisimamisha Uchaguzi Mkuu wa Simba kwa hoja kuwa klabu hiyo inatakiwa kuunda Kamati ya Maadili ili kushughulikia masuala yote yanahusu maadili kabla ya kuendelea na uchaguzi huo, lakini Rage anadhani kuwa uchaguzi huo hauna budi kuendelea kama ulivyopangwa kwa manufaa ya klabu hiyo na soka la Tanzania kwa ujumla.

“Tusisimamishe uchaguzi. Hatutatenda haki kwa Klabu ya Simba kwa sababu maandalizi kwa ajili ya uchaguzi huo yalianza muda mrefu uliopita,” alisema Rage na kuongeza: “Nafahamu (Malinzi) ana mamlaka ya kusimamisha uchaguzi, lakini namwomba kufikiria upya uamuzi wake huo kwa manufaa ya klabu,” alisema Rage.

Rage pia alisema amemwomba Rais huyo wa TFF kwamba klabu haitakuwa tayari kuunda Kamati ya Maadili kuamua suala la mgombea wa urais, Michael Wambura kwani suala lake linahusisha mambo aliyofanya akiwa kiongozi wa chama cha soka nchini, FAT.

“Tuhuma dhidi ya Wambura ni za msingi sana. Baadhi yake zinahusu wakati akifanya kazi FAT. Nimerudisha suala hili kwake,” alisema mbunge huyo wa Tabora Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi.

Kwa miaka kadhaa, Wambura amekuwa akituhumiwa kwa kile kinachojulikana kama ukosefu wa maadili, tuhuma zinazofanya juhudi zake kuwania nafasi mbalimbali katika uongozi wa soka kugonga mwamba.

Zaidi ya hapo, Rage alisema kulikuwa na tuhuma kutoka kwa wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji isipokuwa watatu.

“Katika hali kama hii hatutenda haki kuunda kamati kujadili suala la Wambura,” aliongeza Rais huyo wa Simba.

Aidha, juzi Kamati ya Uchaguzi ya Simba ilikataa agizo la Malinzi ikidai kuwa hana mamlaka ya kufanya hivyo na kwamba uchaguzi uko pale pale, huku ikimwengua kwa mara nyingine, Wambura kuwania Urais kwa madai ya kuanza kampeni kabla ya wakati.

Katika hatua nyingine, Wambura jana aliwasilisha rufaa kwa Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF kupinga kuenguliwa kwa mara nyingine.

Wambura alithibitisha jana kuwa amekata rufaa hiyo akipinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi wa Simba kumwengua kwa madai ya kuanza kampeni kabla ya wakati.

Wakati huo huo, Rage alisema kitendo cha Shomari Kapombe kukataa kujiunga na klabu yake ya Ufaransa, kinaondoa uwezekano wa Tanzania kuja kuwa na wanasoka wa kulipwa barani Ulaya siku za usoni.

Alisema uamuzi wa beki huyo wa kimataifa wa Tanzania umeharibu sura ya Tanzania katika bara hilo.

Kapombe aliruhusiwa kujiunga na Taifa Stars, lakini ameamua kutorejea tena Ufaransa ambako alipelekwa na Simba katika klabu ya AS Cannes na sasa inadaiwa amesajiliwa na mabingwa wa Bara, Azam FC.

Rage alisema alikubali kumuuza Kapombe kwenye klabu ya AS Cannes ya Ufaransa kwa masharti Simba itakapata asilimia 40 ya fedha zitakazopatikana kama atauzwa kwa klabu nyingine.

KLABU ya Simba  imetambulisha  mashindano mapya ya Super  Cup, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi