loader
Raha ya Krismasi ni upendo na uwajibikaji

Raha ya Krismasi ni upendo na uwajibikaji

MWINJILISTI na mtu ambaye katika maisha yake amekuwa akipeleka neno la matumaini kwa wale waliovunjika, Ruth Carter Stapleton anasema Krismasi inakuwa Krismasi ya kweli pale tunapoisherehekea kwa kupeleka upendo kwa wale wanaouhitaji zaidi.

Naam, kesho ni Krismasi na kama utakuwa unaangalia sana maana ya maneno haya Krismasi maana yake ni rahisi sana ni upendo kwa wahitaji.

Ukiangalia maisha ya nchi yetu na wakazi wake utabaini kwamba upendo unaohitajika si kwa wale maskini pekee lakini upendo kwa nchi yetu na uwajibikaji kwani kama yalivyo mataifa mengine tunapita katika magumu kuanzia umaskini , afya na juhudi za kuleta elimu dunia na elimu ahera kwa watu kwa ajili ya mustakabli wa watu kuwa kamili kiafya katika roho na mwili.

Tunapoadhimisha kuzaliwa kwake Yesu Kristo katika hori la wanyama katika mji wa Bethlehemu rtunapaswa kujifunza upendo kwani 

ishara nyingi za uzazi wake zilihitaji kutimiza upendo hasa kwa wahitaji.

Kuwapo kwa Sherehe ya Krismasi zilizoanzia huko Roma mnamo 336, ni juhudi za kimataifa za kusambaza upendo na kukumbuka maana ya kuzaliwa upya katika roho na mwili. Sherehe japo ilianzia mwaka 336 tunaelezwa katika historioa ilishika kasi karne ya 9.

Krismasi kwa waamini husherehekewa kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu Kristo, ambaye Wakristo wanaamini kuwa ni Mwana wa Mungu kunaweza kuwa na maana kwa kuangalia dhana halisi ya ujio wa Kristo duniani.

Hadithi ya kuzaliwa kwa Yesu ni ya kushangaza: Naam ! Ni ya kushangaza kwa kuwa Mungu alitaka wanadamu kujifunza kitu, kujifunza upendo na kunyenyekea. Hebu fikiria, Yeye, Mwana wa Muumba (ndivyo tunavyoamini) , ilibidi azaliwe katika zizi la wanyama.

Mwinjili Luka anasema: “Yusufu pia alitoka Galilaya, mji wa Nazareti, akaenda Yudea, kwa mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa sababu alikuwa wa nyumba na familia ya Daudi, kuandikishwa na Mariamu, mkewe aliyeolewa, ambaye alikuwa mjamzito. walikuwako, wakati wa kuzaa kwake ulifika, naye akamzaa Mwanawe 

wa Kwanza, akamfunga kwa kitambaa, na kumlaza horini, kwa sababu hawakuwa na nafasi yao katika nyumba ya wageni. “ (Luka 2: 4-7)

Ndivyo inavyokuwa mara nyingi hatutoi nafasi katika mioyo yetu kwa wahitaji na katika hili tumekuwa tukichochea chuki, lakini fikiria bwana wa ulimwengu anavyokuja duniani akifunza kusaidia wahitaji.

Kiukweli Uzazi wa Kristo ambao kwa sasa huadhimishwa mara mbili kwanza huu unaofanyika kesho na ule wa wakristo wa Mashariki ambao huadhimishwa Januari 7 una maana kubwa ya daraja la wanadamu na Mungu kupitia amri yake ya upendo.

Mimi naamini kimsingi Sikukuu hii inakumbusha sana upendo kwani Mungu alimtuma Mwanawe, Yesu Kristo, katika ulimwengu huu wenye dhambi kuokoa wanadamu kutoka kwa dhambi na uharibifu wa milele.

Tukifahamu ukweli wa ujio wa Kristo duniani ambao umesababisha hata mpangilio wetu wa matukio huanza na Kuzaliwa kwake Yesu Kristo tunaweza kutekeleza wajibu wetu eneo lolote lililopo kwa weledi na uaminifu mkubwa kwa sababu Mungu wetu ni mwaminifu.

Na pengine katika kujifunza upendo pia tunajifunza kitu tutakachofanya mwaka wa kesho,sensa, hakika inatubidi tuhesabiwe kama sababu iliyofanya Yesu kuzaliwa Bethlehemu.

kwa wasiojua ni kwamba sababu ya Mariamu na Yusufu, wakati huo walikuwa wakiishi Nazareti, kwenda Bethlehemu, ilikuwa sensa. Kulingana na agizo la Kaisari Augusto, kila mkazi wa Dola ya Kirumi alipaswa kwenda “kwa mji wake” ili kuwezesha shughuli ya sensa. Kwa kuwa Yusufu alikuwa wa ukoo wa Daudi, alikwenda Bethlehemu kwa ajili ya Sensa.

Tunapohimizwa upendo ambao ndio unahimili maisha mema na yenye kukinai pia tunapaswa kutambua wajibu wetu katika jamii na katika taifa kufanikisha mambo ambayo ni muihimu katika taifa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/bb45cce0b59bc2f218a04cabf906650a.jpeg

SERIKALI kupitia Shirika ...

foto
Mwandishi: Beda Msimbe

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi