loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ray C atoa ushuhuda dawa za kulevya

Pia kilo 966.06 za dawa za kulevya aina ya heroini, kilo 363.7 za kokeni , kilo 45,734 za mirungi na tani 212.71 za bangi zilikamatwa katika kipindi hicho.

Vilevile watanzania 178 wanatumikia vifungo mbalimbali nchini china katika kipindi cha kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka jana huku wengine 113 wamefungwa Brazil hadi Aprili mwaka huu kutokana na kujihusisha na biashara hiyo ya dawa za kulevya na kuhukumiwa nchini humo.

Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal aliyasema hayo jana kwenye maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya duniani na kubainisha kuwa hali hiyo inaleta taswira mbaya kwa Tanzania kimataifa.

Aidha alisema katika kipindi cha mwaka 2011 hadi Mei mwaka huu kulikuwa na jumla ya watumiaji 1,526 wa dawa za kulevya waliokuwa wanaendelea kupatiwa tiba kwa kutumia dawa aina ya Methadone katika hospitali ya taifa ya Muhimbili,Mwananyama na Temeke.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi alisema vita dhidi ya dawa za kulevya inapaswa kuwa ya watu wote pasipo kubagua umri kwani hivi sasa watu wote wakiwemo watoto wadogo wanatumika katika kusambaza na kusafirisha.

Akitoa ushuhuda wa athari za matumizi ya dawa za kulevya, msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila maarufu kama Ray C mbele ya mamia ya watu waliohudhuria maadhimisho hayo alisema mafanikio makubwa aliyoyapata ikiwemo kujenga nyumba nzuri na ya kisasa akiwa na umri mdogo kutokana na kazi ya muziki yalififia na kubaki historia baada ya kutumbukia katika dimbwi la matumizi ya dawa hizo hatari.

Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili ...

foto
Mwandishi: Joachim Nyambo, Mbeya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi