loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

RC ahimiza ulipaji kodi kwa usahihi

Ulipaji huo wa kodi utaiwezesha serikali kupata mapato na kuweza kutekeleza mipango yake kwa wakati kama ya kuboresha huduma za afya, elimu, miundombinu mbalimbali, ulinzi na usalama.

Aliyasema hayo jana katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Manju Msambya wakati akifungua semina ya walipa kodi wakubwa na wa kati iliyofanyika jijini hapa.

Kwa upande wake, Naibu Kamishna wa Walipa Kodi Wakubwa, Alfred Mregi alisema washiriki wa semina hiyo watapitia sheria mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya mwaka 2014.

Alisema sheria mpya ya VAT imeboreshwa katika maeneo mbalimbali kwa kuyaangalia maeneo yenye mapungufu katika sheria wanayoitumia sasa kama watakavyoelezwa na wataalamu.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Grace Chilongola, Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi