loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

RC aipongeza Airtel kwa maboresho

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ufunguzi wa duka kubwa la kampuni hiyo mjini Dodoma baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa ili liweze kuwa la kisasa linalokidhi mahitaji ya mji mkuu.

Mkuu huyo wa mkoa wa Dodoma pamoja na kuwapongeza kwa kuboresha utoaji wa huduma za mawasiliano kwa watumiaji nchini, amewataka wakazi wa Dodoma kutumia nyenzo hiyo muhimu katika kuunganisha jamii na kuendesha shughuli za kibiashara na kiuchumi .

“Serikali inaunga mkono juhudi zinazofanywa na Airtel na tunawaomba waendelee kuwekeza zaidi katika kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano nchini. Tuko tayari kushirikiana Airtel katika kuhakikisha tunaweka mazingira bora ya kuendesha biashara ili kuwawezesha wananchi wetu kufaidika na huduma hizi za mawasiliano na hatimaye kuwa maisha bora,” alisema Dk Nchimbi.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa wateja Adriana Lyamba alisema:”Leo tunazindua rasmi duka hili lenye muundo mpya lililopo katika barabara ya Mkuu hapa Dodoma ikiwa ni moja kati ya mikakati yetu ya kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zetu na kupunguza msururu wa wateja wanaoingia dukani hapa kupata huduma mbalimbali. “ alisema.

Aidha alisisitiza kwamba kupitia duka hilo wateja watapata huduma za pesa mkononi za Airtel Money ,intaneti na kuweza kununua muda wa maongezi pamoja bidhaa zikiwemo simu za mkononi na vifaa vya huduma za mawasiliano na huduma nyingine nyingi.

Lyamba pia alisema Airtel imeendelea kuboresha maduka yake nchini ambapo hivi karibuni imezindua maduka yake mapya katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza Mbeya na Mtwara.

Maduka mengine yaliyopo Morogoro, Bukoba na Zanzibar yanategemewa kuzinduliwa kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Septemba.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi