loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

RC akiri Watanzania wakijituma hufanya mambo makubwa

Sadik amesema, Watanzania wakithubutu wana uwezo wa kufanya mambo makubwa ikiwa ni pamoja na kuweza kumudu ushindani kutoka kwa wageni ambao zamani walitawala baadhi ya biashara nchini.

Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam kabla ya kuzindua duka kubwa la kampuni ya kizalendo ya TSN Group. Kiongozi huyo wa serikali aliipongeza kampuni hiyo kwa kuboresha maisha ya Watanzania na kujenga uchumi wa nchi.

“Watanzania wakiamua wanaweza, Watanzania wakipewa fursa wanaweza wakafanya mambo makubwa…ninyi hapa mmepita katika mawimbi makubwa lakini mmehimili mpaka sasa mmeweza kufungua duka hili la sita,” alisema na kuipongeza kampuni hiyo kwa kuajiri zaidi ya Watanzania 450 hadi sasa.

Alisema, wakati wa kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu uliopita, aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete aliahidi kuwawezesha wananchi kupata ajira, na kwamba, ahadi hiyo inatekelezwa kwa vitendo na wawekezaji wazalendo.

Sadiki alisema, ajira katika kampuni hiyo ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM hivyo wananchi nao waunge mkono juhudi za wawekezaji wazalendo ili wananchi wengi zaidi wapate ajira.

Aidha Sadiki ametoa changamoto kwa maduka makubwa nchini kuacha kuthamini zaidi kutoka nje, wauze na zile zinazozalishwa na wananchi au viwanda vya ndani zenye ubora unaohitajika.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TSN Group, Farough Baghozah, alisema, hakuna njia ya mkato kupata mafanikio na amepinga kauli inayotumiwa hasa na vijana ya kusema ‘nitoke vipi’.

“Hakuna njia ya mkato katika maisha, ni kujituma na kuwa mwaminifu ndiyo unaweza kubadilisha maisha yako,” alisema na akatoa wito kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo wawe waaminifu na watoe huduma bora.

WAZIRI wa Maendeleo ya Nishati na ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi