loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

RC aonya watakaopaisha bei za bidhaa mwezi mtukufu

Alitoa kauli hiyo katika mkutano wake na waandishi wa habari jana na kuwataka wafanyabiashara wa vyakula kuondoa tamaa na vishawishi vitakavyopelekea kupandisha holela bei ya vyakula.

Alisema miaka mitatu iliyopita mkoa uliunda kamati ya udhibiti wa bei ya vyakula wakati wa mwezi wa Ramadhani na imewezesha wafanyabiashara kutopandisha holela bei ya vyakula kwenye masoko mbalimbali.

“Wafanyabiashara wasimame katika angalizo na hakuna kupandisha bei ya vyakula na kila moja anatakiwa kuzingatia hilo” alisema Pia aliwataka wafanyabiashara kuacha tabia ya kuficha vyakula na kusubiri vipande bei. “Hata wasiofunga wamekuwa wakiathirika na bei ni vizuri wafanyabiashara wakafikiria hilo ili wananchi wasiathirike na mfumko wa bei za bidhaa mbalimbali” alisema.

Kwa upande wake, mfanyabiashara ya viazi mviringo katika Soko kuu la majengo Mjini hapa Abubakar Athumani, alisema bei ya viazi imepanda kutokana na wakulima kuanza kupandisha bei taratibu.

Alisema amekuwa akichukua viazi kutoka mikoa na Mbeya na Njombe na kuleta Mkoani Dodoma na kuuza kwa wafanyabiashara.

Alisema katika kipindi cha mfungo mahitaji ya viazi yamekuwa makubwa na mkulima anapoamua kupandisha bei hawana la kufanya. Alisema kwa sasa bei ya viazi kutoka Njombe ni Sh. 60,000 hadi Sh. 65, 000 kwa gunia la kilo 100 na viazi kutoka Mbeya vimekuwa vikiuzwa Sh. 70,000 hadi Sh 75,000 kwa gunia la kilo 100 ambapo wastani ya kilo moja ya viazi ni Sh. 700.

Mfanyabiashara wa viazi, mihogo, magimbi na nazi katika soko la Majengo, Abdul Ngalawa alisema bei ya bidhaa imekuwa ikipanda kidogo kidogo na wanaoleta bidhaa sokoni hapo kutoka mikoani wamekuwa wakidai wanakochukulia bidhaa hizo bei imepanda.

Alisema sasa gunia moja la mihogo wamekuwa wakiuziwa Sh. 55, 000 kutoka Sh. 50,000. Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu wa Soko Kuu la Majengo, Idd Vumba alisema bado bei ya bidhaa katika soko hilo ni kawaida.

RAIS John Magufuli amewataka wasaidizi wake ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi