loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Real Madrid yaacha gumzo Kilimanjaro

Msafara wa nyota hao, uliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro saa 6:15 mchana kwa ndege ya Fast Jet namba 5H-FJA, huku mamia ya wapenzi na mashabiki wa soka wakimiminika kwa wingi kushuhudia miamba hiyo ikipita.

Wakati msafara huo ukitoka KIA, mashabiki hao walijipanga barabara kuu ya Arusha- Moshi iliyokuwa imefungwa huku wakipeperusha bendera za taifa kuonesha uzalendo wa nchi yao.

Msafara huo ulielekea katika hifadhi za mlima Kilimanjaro (KINAPA), ambapo wachezaji hao walipata muda wa kuzuru kwa kiasi cha mita 400 kujionea mlima huo ambao ni mrefu kuliko yote Afrika kwa kupitia njia ya Marangu.

Pia walizuru maporomoko ya maji ya Marangu yaliyo na urefu wa mita 200, hali iliyowafanya wageni hao kupiga kelele za shangwe walipojionea maporomoko hayo ya ajabu.

Akizungumza na gazeti hili mmoja wa nyota hao, Miguel Palencia aliyekuwa akicheza beki ya kulia kati ya mwaka 2002-2005, alisema amejisikia vizuri kutembelea Tanzania, hususani mkoa wa Kilimanjaro na kujionea mlima na maporomoko ya maji, kitu ambacho kimempanua zaidi ufahamu.

Kwa upande wake nahodha wa Real Madrid, Andres Sabido alisema Tanzania ni nchi nzuri inayovutia hata kwa kuitazama, huku akisisitiza kujituma katika kuendeleza nchi ni jukumu la Watanzania wenyewe huku wakijifunza kutoka kwa mataifa mengine yaliyofanikiwa zaidi.

Nyota hao waliambatana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara.

Nyota hao walishuhudia mechi kati ya Panone FC (Ligi daraja la kwanza) na Machava FC (Ligi daraja la tatu) ambapo Panone ilishinda bao 1-0 katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Ushirika.

foto
Mwandishi: Arnold Swai, Moshi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi