loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Redio Jamii ya Tumbatu yazinduliwa

Mbarouk alisema redio jamii zimekuwa chachu ya kuleta maendeleo ya mabadiliko mbalimbali katika maeneo yao na kuwataka wananchi kuzitumia vizuri.

“Tangu kuanza kufunguliwa kwa redio jamii katika maeneo mbalimbali ya Pemba, tumegundua yapo mafanikio makubwa na mabadiliko katika sekta mbalimbali,” alisema.

Awali, Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi aliutaka uongozi wa redio jamii ya Tumbatu, kutoa elimu itakayosaidia wananchi kupambana na uvuvi haramu, ambao umekuwa tishio kwa uharibifu wa rasilimali za baharini.

Alisema hivi sasa kumejitokeza wimbi la uvuvi haramu, licha ya juhudi za Serikali kukabiliana na tatizo hilo, ambalo linaonekana wazi ni kuwepo kwa tamaa ya wavuvi kupata mapato ya haraka katika kipindi cha muda mfupi.

“Tunaitaka Redio jamii ya Tumbatu ilete mabadiliko makubwa na kutoa Elimu ya uhifadhi wa mazingira kukabiliana na athari za uvuvi haramu katika maeneo ya hifadhi,”alisema Balozi Seif.

Alisema Redio nyingi za jamii zilizoanzishwa Unguja na Pemba zimeweza kuleta mabadiliko na kubadilisha maisha ya wananchi kwa kutoa Elimu pamoja na kupambana na umasikini.

Mapema, Ofisa Tawala wa kisiwa cha Tumbatu ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Redio jamii, Mohamed Omar alisema Redio hiyo itakuwa ikitayarisha vipindi vyenye kutoa elimu ya mambo mbalimbali na maendeleo kwa shule za msingi na vyuo vya madrasat.

Kwa mfano, alisema bado elimu inahitajika kwa wananchi wa Tumbatu pamoja na akinamama kuzitumia huduma za afya katika hospitali hiyo pamoja na kujifungua.

“Bado akinamama wengi hawajazitumia ipasavyo huduma za afya na uzazi salama kwa lengo la kupunguza vifo vya watoto wachanga,” alisema.

Mapema, Ofisa Mwandamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la (UNESCO), Abdulwahabi Karibai akitoa salamu zake, alisema Redio jamii lengo lake kuelimisha wananchi wanaoishi maeneo hayo na kuleta mabadiliko.

“Redio jamii hizi zikatumiwa vizuri zinaweza kuleta mabadiliko makubwa ya maisha ya watu na kupata taarifa mbalimbali muhimu kwa maendeleo ya Taifa,” alisema.

Zipo jumla ya Redio jamii tatu Zanzibar na Redio jamii ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba na Mtegani iliyopo Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.

Redio jamii iliyopo Micheweni Pemba, ambayo ni ya kwanza kwa upande wa Zanzibar, inatajwa kupata mafanikio makubwa kwa kusaidia kuelimisha wananchi wa wilaya hiyo, ambao walikuwawapo nyuma katika masuala ya jamii pamoja na chanjo kwa watoto na akinamama na ajira mbaya za watoto, ambazo zilisababisha wanafunzi kuacha shule.

MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi