loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Robben: Nilijiangusha

Klaas-Jan Huntelaar alifunga bao la ushindi la mkwaju wa penalti katika dakika za nyongeza baada ya Robben kufanyiwa madhambi. Kocha wa Mexico, Miguel Herrera amemtuhumu Robben kwa kujiangusha mara tatu katika mechi hiyo, lakini mshambuliaji huyo aliiambia luninga ya Uholanzi:

“Naomba radhi, katika kipindi cha kwanza nilijiangusha.”

Robben alifanyiwa madhambi na nahodha wa Mexico, Rafael Marquez katika dakika ya 94, lakini Herrera anasema mchezaji huyo wa Bayern Munich hakupaswa kuwepo uwanjani kutengeneza penalti. “Robben alijiangusha mara tatu,” alisema kocha huyo.

“Unaweza kujiuliza juu ya mchezaji huyu anayejaribu kudanganya, kama Robben alifanya hivyo tena, alipaswa kupewa kadi nyekundu.”

Awali, Mexico ilihofia kupigiwa penalti katika kipindi cha kwanza baada ya Robben kuangushwa ndani ya eneo la hatari akiwania mpira na Hector Moreno.

Mwamuzi wa Ureno, Pedro Proenca alipeta na kuashiria mchezo uendelee ambapo mapema kipindi cha pili Mexico wakapata bao la kuongoza likifungwa na Giovani Dos Santos. Robben akaanguka tena ndani ya eneo la hatari baada ya kuwania mpira na Miguel Layun kabla Wesley Sneijder hajafunga bao la kusawazisha.

Mechi ikiwa kwenye dakika za nyongeza, Robben aliangushwa ndani ya eneo la hatari na mwamuzi aliamuru penalti ambapo Huntelaar hakufanya makosa na kuivusha Uholanzi kwenye hatua ya robo fainali.

Marquez alidai kuwa baada ya mechi Robben alikiri kuwa mwenye bahati na maamuzi yale. Beki huyo wa zamani wa Barcelona, Marquez alisema:

“Nilizungumza na Robben baada ya mechi akaniambia kwamba haikuwa penalti.” “Alisema rafu aliyofanyiwa mwanzo ilikuwa penalti, lakini ile haikuwa penalti.”

Wakati huo huo, Rais wa Uruguay, Jose Mujica ameiita Fifa kikundi cha wahuni kutokana na uamuzi wao wa kumfungia Luis Suarez miezi minne.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 79, ameielezea adhabu aliyopewa Suarez ambayo pia inajumuisha na kutocheza mechi tisa za kimataifa kuwa ‘adhabu kandamizi’. Suarez ameweka historia kwenye Kombe la Dunia baada ya kumng’ata beki wa Italia, Giorgio Chiellini.

Ametoa kauli hiyo kwenye luninga ya taifa wakati wa mapokezi ya timu ya Uruguay iliyoondolewa hatua ya mtoano na Colombia. Rais alizungumza hayo na kuwaambia waandishi wa habari kuyaandika, alipoulizwa kama anataka yaandikwe.

Alisema Suarez amepewa adhabu hiyo na Fifa kutokana na historia yake ya maisha.

Pia ameilezea adhabu hiyo kama aibu kubwa kwa historia ya Kombe la Dunia. Kikosi cha Oscar Tabarez kilifungwa mabao 2-0 na Colombia baada ya kulazimika kucheza bila mshambuliaji wake anayetumikia kifungo, Suarez. Uruguay wamekata rufaa Fifa.

MCHEZO wa Ligi Kuu ya Soka la Wanawake kati ya ...

foto
Mwandishi: BRASILIA, Brazil

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi