loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rose Muhando kuzindua albamu mpya leo

Akizungumza na gazeti hili, Muhando alisema maandalizi yote muhimu kuhusu albamu yake yamekamilika na kuwaomba mashabiki wake kujitokeza kwa wingi.

“Nimejipanga kuwapa furaha mashabiki wangu, waje tujumuike pamoja kuzindua albamu yangu,” alisema Muhando.

Alisema albamu hiyo ina nyimbo za Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu na Facebook.

Alisema baada ya uzinduzi wa leo ambao mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, atakwenda kuitambulisha mkoani Tabora Agosti 8 na siku inayofuata itatambulishwa Geita wakati Agosti 10 itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Baadhi ya waimbaji mahiri wanaotarajiwa kusindikiza uzinduzi huo ni Upendo Nkone, John Lissu, Bonny Mwaitege, Upendo Kilahiro, Sarah K na Ephraim Sekeleti.

Licha ya albamu yake ya Utamu wa Yesu, pia Muhando amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi), Jipange Sawasawa, Kitimutimu, Mungu Anacheka na Wololo.

KOCHA wa timu ya taifa, ‘Taifa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi