loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

RT wapokea hotuba ya JK kwa msisimko

Juzi Rais Kikwete katika hotuba yake hiyo Ikulu, Dar es Salaam, aliwataka viongozi wa RT kuwa na mikakati endelevu itakayosaidia kuendeleza mchezo wa riadha nchini na ushiriki wa michezo ya kimaitaifa ikiwamo ya Madola ambayo kifimbo hicho ni miongoni mwa hatua za kuelekea michezo hiyo.

Rais alisema viongozi wa RT wamekuwa wakichelewa kuandaa timu na kuanza maandalizi yao ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa michezo husika.

Akizungumzia hotuba hiyo, Rais wa RT, Anthony Mtaka alisema kwa upande wa chama hicho wameipokea hotuba hiyo kwa mikono miwili na imetoa mwanga kwa mustakaballi wa chama hicho. Mtaka alisema ni hotuba ambayo mbali na kukichambua chama cha RT, lakini pia ni wakati muafaka kwa wale ambao wameombwa msaada na chama hicho kuanza mchakato wa kukisaidia.

Alisema RT inahitaji fedha za maandalizi ya timu ya Taifa ya riadha ambapo Sh milioni 300 zinahitajika. Alisema kwa sasa mchanganuo mzima wa namna ambavyo fedha hizo zitatumika upo kwenye Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na wanasubiria fedha ili waanze kazi.

Alisema tayari mchakato wa kutafuta wachezaji watakaoshiriki michuano hiyo ya Jumuiya ya Madola imeshakamilika na kwa sasa kinachosubiriwa kwa sasa ni kuanza kwa kambi.

Alisema Februari 9, mwaka huu kutakuwa na kikao cha awali cha kujadiliana uendeshaji wa kambi hiyo itakayofanyika Hombolo mkoani Dodoma.

Alisema wanariadha hao wataweka kambi hiyo katika Chuo cha Serikali za Mitaa kilichopo katika eneo hilo la Hombolo, lakini kwa baadaye watahamia Babati.

Alisema mikakati yote hiyo ili kufanikiwa, inahitaji fedha na aliongeza kuwa kwa kupitia hotuba ya Rais Kikwete, wadhamini wajitokeze na pia wanaotakiwa kutimiza majukumu kwa upande wao wafanye hivyo.

“Sisi kazi yetu ni kuandaa timu ambapo tayari tumeshaifanya na kwa sasa ni upande wa pili ambao ni wa kusaidiwa kufanikisha kambi hii, msaada ambao kila mdau anakuwa na jukumu lake la kutimiza na kwa sasa naona kuwa ni vema hilo likafanyika,” alisema Mtaka.

Aliongeza kuwa wamepata wachezaji kutoka katika Jeshi la Polisi, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, sekondari na wachezaji wa timu za Taifa waliopita.

Alisema katika hotuba ya Rais ambapo alisisitiza kuwa maandalizi ya timu hiyo ni muhimu na inatakiwa yafanyike mapema kwa upande wake anaona kuwa RT imeshafanya maandalizi yake na hivyo anaomba upande wa pili wa msaada utakaofanikisha kambi utimizwe mapema ili kambi ianze mapema. Julai 23, mwaka huu, Michezo ya Jumuiya ya Madola itaanza Glasgow, Scotland hadi Agosti 3, mwaka huu.

KLABU ya Simba  imetambulisha  mashindano mapya ya Super  Cup, ...

foto
Mwandishi: Evance Ng'ingo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi