loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rufaa ya mke aliyetaka kumuua mumewe

Jaji Mwaimu alisema kesi hiyo ilikuwa na mawakili wawili waliopita, lakini katika jalada hakuna sehemu iliyoandikwa sababu za kujitoa kwa mawakili hao.

Alisema yeye kuendeleza kusikiliza na kutoa maamuzi ya rufaa hiyo ni ukiukwaji mkubwa wa kisheria.

Wakili Glorie Ojare alimweleza Jaji Mwaimu kuwa walifanya jitihada za ziada za kusaka mawakili wa awali, Fidelis Peter na Samsoni Rumende katika simu zao za kiganjani, lakini ilishindikana kutokana na simu zao kufungwa.

Jaji alisema hataweza kusikiliza rufaa hiyo na alirudisha jalada kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kanda ya Arusha, Stella Mugasha aipangie kesi tarehe nyingine.

"Siwezi kusikiliza tena kesi hii kwa sasa mpaka wale mawakili waliojitoa waje mbele ya mahakama hii kujieleza kwa mdomo ama kwa maandishi juu ya kujitoa kwao na sasa jalada hili ninalirudisha kwa Jaji Mfawidhi ili aweze kulipangia tarehe nyingine,’’alisema Jaji Mwaimu.

Awali Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilitupilia mbali ombi la hati ya dharua ya dhamana ya mwanamke huyo kwa madai kuwa wakili wa awali, Rumende alikosea kisheria namna ya kukata rufaa hiyo. Janeth na Novatus Elias kwa pamoja wanatuhumiwa kupanga njama za kutaka kumuua mumewe wa ndoa na mtoto wa mume huyo.

Awali, Mahakama ya Wilaya mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Devota Kamzola ilimyima dhamana mshitakiwa kwa madai kwamba kuitoa ni kuvuruga upelelezi wa kesi hiyo, kwani baadhi ya watuhumiwa hawajakamatwa.

Katika hati ya mashitaka, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Edna Kasala alidai washitakiwa wote wawili walitaka kumuua Desderi Sabas ambaye ni mtoto wa nje wa mume huyo anayeishi Bukoba mkoani Kagera.

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi