loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rushwa inaumiza wajawazito

Malalamiko juu ya kero ya rushwa katika vituo vya umma jijini Dar es Salaam inazidi kuongezeka kila kukicha kutokana na madai ya wajawazito kuwa hulazimishwa kutoa kati ya Sh 15,000 hadi 200,000 ili kupata huduma afya ya uzazi salama.

Mambo yanayosababisha wanawake kutoa hongo kwa baadhi ya madaktari ni pamoja na mtoto kukaa vibaya na mtoto kufia tumboni ambapo wajawazito hulazimika kutoa rushwa ili kuokoa maisha yao.

Madai mengine ni kitendo cha wauguzi na wakunga kuchelewa kuwapatia huduma wajawazito waliyofikia hatua ya kujifungua. Ucheleweshaji huo hufanywa na baadhi ya wauguzi ambao huwabeza wajawazito kwa madai kuwa wanadeka au wanapiga kelele za maumivu ya uchungu kama mbinu za kutaka kupapaswa.

Serikali na wadau wa afya ya uzazi salama wanapaswa kukemea rushwa na unyanyasaji dhidi ya wajawazito unaofanywa na baadhi ya wakunga na wauguzi katika hospitali na vituo vya afya nchini.

Ikiwezekana Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ianzishe mpango shirikishi kwa njia ya simu kutoa taarifa kuhusu wauguzi na wakunga wanaochelewesha huduma ya afya ya uzazi kama njia ya kushinikiza wajawazito kutoa rushwa.

Ikiwezekana wizara ya afya iweke utaratibu maalumu wa kukusanya matukio ya wanawake na watoto wanaokufa wakati wa uzazi ili kujua hospitali na vituo vya afya vinavyokabiliwa na vifo vingi na kuchunguza chanzo cha vifo hivyo ili kubaini kama vimetokana na uzembe au la.

Ni vyema sehemu za huduma ya afya ya uzazi ziwekwe masanduku ya kutolea maoni na malalamiko.

UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Riadha ...

foto
Mwandishi: Kanaeli Kaale

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi