loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

'Ruvuma ibueni fursa za kiuchumi'

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Raymond Mbilinyi alitoa mwito huo kwa wajumbe wa Baraza la Biashara la Mkoa wa Ruvuma hivi karibuni mjini hapa.

Alisema wakati umefika kwa halmashauri kuainisha maeneo yote muhimu yenye fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji.

“Mkutano huu na wadau wote wa baraza ambao unawajumuisha wajumbe kutoka halmashauri zote za mkoa huu ni vyema mnaporudi kwenye maeneo yenu ya kazi mkafanya mchakato wa kuainisha fursa zote,” alisisitiza Mbilinyi.

Alisema Baraza linaamini endapo halmashauri zitaibua fursa za biashara mapato ya Serikali yataongezeka.

Pia ajira kwa vijana zitaimarika hivyo kipato kwa Watanzania kukua. Katika kikao na waandishi wa habari, Mbilinyi alisema “Huu mkoa una kila sababu za kujivunia katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara kwani una ardhi ya kutosha yenye rutuba na mvua ya kutosha pia.”

Alisema mbali na kilimo, Mkoa wa Ruvuma una madini ya urani, makaa ya mawe na maeneo mazuri ya kuvutia utalii wa ndani na nje ya nchi.

“ Mkoa huu ni tajiri sana, kila kitu kipo jambo kubwa ni kwa watendaji wa halmashauri kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara na kuvutia zaidi uwekezaji katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kubadilisha maisha ya watu,” alisema.

Alisema kuwepo kwa Baraza la Mkoa ambalo linajumuisha wajumbe kutoka sekta za umma na binafsi, itakuwa chachu kubwa ya kuongeza kasi ya kimaendeleo katika wilaya zote mkoani hapa.

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Ernest Kahindi, alisema wilaya yake inategemea uvuvi kuingiza kipato katika halmashauri hiyo na kusema kuwa lengo lao kwa sasa ni kuwawezesha vijana kwa kuwapatia zana za kisasa za kuvulia samaki.

Mwenyekiti wa Chama cha wenye Viwanda Biashara na Kilimo ( TCCIA) Wilaya ya Tunduru Mohamed Kiondo alisema Baraza hilo limewapa mwamko katika kuhimiza kilimo katika wilaya zao.

Alisema mkoa unategemea kilimo hususani tumbaku, korosho na mahindi ambayo kwa mujibu wake, mazao hayo yanaingiza fedha nyingi. “Baraza hili ni fursa pekee ya kujitangaza,” alisema Kiondo.

MCHICHA ni aina nyingine za ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Songea

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi