loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Saba zathibitisha ushiriki bonanza Shimmuta

Kwa mujibu wa taarifa Katibu Mkuu wa Shimmuta, Award Safari, uthibitisho huo ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika mkutano wa pamoja kati ya viongozi wa timu zilizoalikwa na viongozi wa Kamati ya Utendaji uliofanyika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) Muhimbili.

Alitaja timu zilizothibitisha kushiriki kabla ya tarehe ya mwisho iliyowekwa Agosti 30, mwaka huu.

Timu hizo ni Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL), Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Chuo Kikuu cha Muhimbili, Chuo Kikuu cha Ardhi, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Safari alisema michezo itakayochezwa katika bonanza hilo itakuwa mpira wa miguu, netiboli, kukimbia ukiwa ndani ya gunia, kula ‘Apple’ likiwa linaning’inia, drafti na bao.

“Kamati ya Utendaji ya Shimmuta inaziomba timu zote zilizoalikwa kwenye bonanza hili zithibitishe mapema ushiriki wao kabla ya Agosti 30, mwaka huu ili taratibu za maandalizi kwa upande wa kamati zikamilike kikamilifu,” alisema.

RUVU Shooting, Kagera Sugar na Gwambina ...

foto
Mwandishi: Sophia Mwambe

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi