loader
Dstv Habarileo  Mobile
Samata, Ulimwengu kuivaa Zimbabwe

Samata, Ulimwengu kuivaa Zimbabwe

Samata na Ulimwengu awali walitangazwa kwamba wasingeweza kufika kucheza mechi hiyo ya raundi ya awali ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani 2015 dhidi ya Zimbabwe kwa sababu walikuwa na majukumu mengine katika klabu yao ya TP Mazembe.

Lakini jana, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lilitoa taarifa kwamba wachezaji hao Samata na Ulimwengu wanatarajiwa kuwasili kesho mchana kujiunga na Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi ya Zimbabwe.

“Washambuliaji hao watatokea moja kwa moja Sudan ambapo kesho (leo, Mei 16 mwaka huu) TP Mazembe itacheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya timu ya huko,” ilisema taarifa ya Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura.

Ilisema kwamba ujio wa washambuliaji hao utafanya wachezaji wote kutoka nje walioitwa na kocha Mart Nooij kuwa wamepatikana kwa ajili ya mechi hiyo ya mchujo ya Afcon.

Mchezaji mwingine wa nje ambaye tayari ameripoti Stars ni Mwinyi Kazimoto anayecheza nchini Qatar.

“Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) linamshukuru Mmiliki wa TP Mazembe ambaye pia ni Gavana wa Jimbo la Katanga, Moise Katumbi kwa kuwaruhusu wachezaji hao kujiunga na Taifa Stars kwa vile mechi dhidi ya Zimbabwe ipo nje ya kalenda ya FIFA,” iliongeza taarifa ya Wambura.

Taifa Stars ambayo ilikuwa Mbeya kwa kambi tangu mwishoni mwa mwezi uliopita, iliwasili nchini juzi na kuendelea na mazoezi  kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikiwa na wachezaji 26.

Kwa mujibu wa Wambura, kocha Nooij atakuwa na mkutano na waandishi wa habari leo utakaofanyika saa 5 kamili asubuhi kwenye
kambi ya Taifa Stars iliyopo katika Hoteli ya Accomondia.

Katika hatua nyingine, Zimbabwe inatarajiwa kuwasili usiku wa kuamkia kesho ikiwa na msafara wa watu 27. Timu hiyo itatua saa 7.30 usiku kwa ndege ya Ethiopian Airlines.

Zimbabwe itafanya mazoezi kesho jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa Jumapili saa 10 kamili jioni kwenye uwanja huo huo.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi