Aidha uzinduzi huo umeenda sanjari na kutoa huduma stahiki na bidhaa halisi za kampuni hiyo zinazouzwa na kupata waranti ya miaka miwili endapo bidhaa hizo zitaharibika.
Hayo yalisemwa jana jijini hapa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo nchini, Mike Seo wakati alipokuwa akizungumza na wauzaji wa bidhaa hizo pamoja na wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa duka hilo.
Alisema lengo la kufungua duka hilo ni kukidhi mahitaji ya wateja wa kampuni hiyo kwani Arusha ni mji wa kiuchumi, kitamaduni pia ni kitovu cha utalii na diplomasia Afrika Mashariki.
Naye Mikidad Mubaraka ambaye ni moja kati ya wadau wa kampuni hiyo, alisema lengo la kuzindua kituo hicho jijini hapa ni kusogeza huduma karibu na wateja na kuboresha mahusiano ili wateja kununua bidhaa halisi badala ya kukimbilia bidhaa feki.
Aliongeza kuwa teknolojia ya Samsung inatumiwa na watu zaidi ya 236,000 kwenye inchi 79 na inaleta mabadiliko na kuiwezesha dunia kuingia kwenye teknolojia mpya ya matumizi ya simu za kisasa na luninga.