loader
Picha

Serengeti Boys hakuna kulala

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Julai 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, timu hizo zilitoka sare ya kutofungana. Ili isonge mbele, Serengeti Boys inahitaji ushindi leo au aina yoyote ya sare ya mabao.

Iwapo itafuzu itaingia raundi ya tatu, ambapo itacheza mechi zake kati ya Septemba 12 na 14, mwaka huu wakati marudiano itakuwa kati ya Septemba 26 na 28, mwaka huu.

Amajimbos kama ilivyo Serengeti Boys, imeingia katika raundi ya pili pamoja na timu za Angola, Benin, Botswana, Burkina Faso, Congo Brazzaville, Ethiopia, Gabon, Ghana, Ivory Coast, Mali, Morocco, Nigeria, Rwanda, Senegal, Tunisia na Zambia.

Kikosi cha Serengeti Boys kinachoongozwa na Kocha Mkuu, Hababuu Omari tayari kiko nchini humo tangu Julai 27, mwaka huu ili kuhakikisha kinasaka ushindi na kuwapa nafasi ya kusonga mbele.

Wakati wanaondoka, Omari alisema matumaini makubwa ni kufanya vizuri katika mchezo huo kwani tayari amerekebisha baadhi ya mapungufu yaliyoonekana katika mchezo wa kwanza.

Katika mchezo huo wa kwanza, Amajimbos walionekana kuwa imara na bora kiufundi wakati Serengeti ilionekana woga ingawa walikuja kubadilika kwa kadiri muda ulivyosogea.

Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Razia Msuya juzi aliitembelea timu hiyo na ile ya Taifa Stars kuzisalimia na kuzihimiza ili kufanya vizuri.

MABINGWA wa kihistoria Yanga leo wanashuka dimbani kuikabili Tanzania Prisons ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi