loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

'Serikali haiwajibiki kulipa mafao ya watumishi wa Tan-Cut-Almasi '

Naibu Waziri alisema kampuni hiyo ilianzishwa kama kampuni ya umma, chini ya sheria ya Makampuni, ikiwa chini ya Shirika Mama la State Mining Corporation (Stamico) miaka ya 1970.

Alisema kampuni hiyo ilianzishwa kuiongezea thamani almasi iliyokuwa ikichimbwa Mwadui isiendelee kuuzwa ikiwa malighafi .

Alisema watumishi hao kama walivyokuwa wengine wa mashirika ya umma hawakuwa watumishi wa serikali, bali ni kampuni husika.

Kwa mujibu wake, kampuni hiyo ilifungwa mapema zaidi ya miaka 10 kabla ya urekebishaji wa Mashirika ya Umma kuanza, hivyo haikuwepo wakati wa kurekebisha mashirika na kuwa watumishi wake hawakuwa wameajiriwa na serikali, hivyo serikali haiwajibiki kuwalipa mafao.

“Serikali inafanya kazi kwa kufuata taratibu na kanuni, TAN-CUT hawakuwa kwenye orodha ya mashirika yaliyoingizwa kwenye zoezi la kubinafsishwa na PSRC, hivyo serikali haiwajibiki kuwalipa mafao”, alisema Mkuya.

Akifafanua uamuzi wa serikali kulipa mafao watumishi wa mashirika ya umma, Waziri anasema ulichukuliwa wakati wa sera ya kurekebisha mashirika ya Umma mwaka 2000 baada ya makubaliano baina ya wafanyakazi, serikali na wawekezaji.

Alisema wawekezaji walipenda kuchukua kampuni bila kuwa na mgogoro wa malipo ya watumishi na kuwa malipo hayo hayakutokana na bajeti ya serikali, bali mapato yaliyotokana na kuuza mashirika, ambayo yalisimamiwa na PSRC.

TANZANIA na Burundi zimetiliana saini makubaliano katika ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi