loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali kukarabati kambi za wazee

Kwa sasa idara hiyo iliyo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ina jumla ya kambi 17 za makazi ya wazee wasiojiweza.

Kati ya hizo, mbili zipo mkoani Morogoro ambazo ni Funga Funga ya Manispaa ya Morogoro, na Chazi katika Wilaya ya Mvomero.

Kamishna wa idara hiyo, Dunford Makala, aliliambia gazeti hili hivi karibuni kwamba, majengo mengi kwenye kambi za wazee wasiojiweza ni machakavu na yanahitaji kufanyiwa ukarabati mkubwa ama kujenga mengine mapya.

Alisema idara imejielekeza katika kuandaa mpango maalumu utakaowezesha kupata fedha kwa ajili ya kukarabati makazi ya wazee wasiojiweza nchini kwa kufanya mazungumzo na baadhi ya wahisani, ambao baadhi wameonesha mwelekeo mzuri.

“Hali ya makazi haya si nzuri sana ...yanahitajika kukarabatiwa ama kujengwa mapya, lakini bajeti haitoshi na mkakati wa idara ni kupata wadau na wafadhili wa kusaidia fedha na tayari wapo walioonesha nia,” alisema Kamishna huyo.

Kamishna huyo wa Idara alitaka wananchi wanaoishi karibu na makazi hayo na wengineo kujitokeza kusaidia wazee hao.

WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi