loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yafagilia ujio wa makocha wa Barca

Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juliana Yassoda kwa niaba ya Waziri Dk Fenella Mukangara wakati akitambulishwa ujio wa makocha hao waliokuwa wakitoa mafunzo ya siku mbili kwa makocha wa Ligi Kuu na Ligi ya Daraja la Kwanza.

Makocha hao wa FC Barcelona ni Daniel Alsina na Isaac Hernandez kutoka Shule ya Soka ya FC Barcelona ambapo wameletwa na klabu hiyo kwa ushirikiano na bia ya Castle Lager, ikiwa ni sehemu ya manufaa ya ushirikiano uliosainiwa mwaka jana kati ya FC Barcelona na bia hiyo.

Yassoda alisema urafiki wa nchi mbili ni jambo kubwa kwani uwekezaji wa pamoja unahitajika katika kuinua michezo sio tu kwa kampuni hiyo, bali na nyingine pia.

“Tukipata makocha wanaotoka katika timu bora duniani, ni faraja kwetu na ni faida kwa makocha wetu kwa niaba ya Serikali, niwapongeze Castle Lager,” alisema.

Balozi wa Hispania nchini, Luis Manuel alisema ujio huo ni muhimu kwa Watanzania na ana matumaini ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo utaendelezwa kwa maendeleo ya michezo.

Naye Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kushillah Thomas alisema ujio wa makocha hao ni ahadi yao katika kuinua soka la Tanzania hivyo wanatarajia makocha wa Kitanzania watatumia ujuzi watakaopewa kuvisaidia vipaji na kuviendeleza katika kiwango cha kimataifa.

“Tunawashukuru makocha wetu wageni, tuna imani makocha wetu wa Tanzania watachukulia kama ni faida kwao kwa kujifunza mbinu ambazo FC Barcelona inazitumia kupata mafaniko,” alisema.

Kocha wa FC Barcelona, Isaac Oriol alisema anashukuru Castle Lager kwa kuwawezesha kufika Tanzania kwani wako hapa kwa ajili ya kuwapa ujuzi makocha wa kitanzania, lakini pia kubadilishana mawazo.

KOCHA wa timu ya taifa, ‘Taifa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi