loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Serikali yajivunia maelfu ya miradi ya maji

Hayo yalisemwa na Waziri wa Maji Profesa Juma Maghembe wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chunyu, Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma, kabla ya kumkaribisha Rais Kikwete kuzindua mradi wa maji katika kijiji hicho.

Profesa Maghembe alisema mradi wa Chunyu ni miongoni mwa miradi 230 iliyokamilika na inatoa maji kwa watu milioni mbili. Pia alisema miradi 538 kwenye vijiji 540 inaendelea kujengwa na itakamilika baada ya miezi sita.

Waziri Maghembe alisema miradi mingine 525 imekabidhiwa makandarasi na kazi ya utekelezaji inatarajia kuanza Oktoba mwaka huu.

Alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2015 watu milioni 7.2 wanapata huduma ya maji. Alisema miradi mingi ya maji katika Mkoa wa Dodoma ilifunguliwa wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji.

Pia aliwataka wananchi kutunza mradi huo kwani ni wao na kuhakikisha maji yanaendelea kutoka. Awali Mbunge wa Mpwapwa Gregory Teu alisema jimbo hilo limekuwa likikabiliwa na kero kubwa ya maji na hata umeme kwa ajili ya kuendeshea miradi ya maji.

Alisema ni vyema kama Serikali ikajenga mabwawa ili wananchi wawe na uhakika wa kupata maji.

“Ujenzi wa mabwawa ni muhimu maji yanatoka milimani na hata Kiteto na kuishia mto Nyasumbi lakini kungekuwa na mabwawa ya maji yangesaidia sana wananchi,” alisema.

Mradi wa maji wa Kijiji cha Chunyu umefikia asilimia 100 na mradi upo katika kipindi cha uangalizi kuanzia Agosti mwaka huu hadi Januari mwakani na baada ya hapo mradi utakabidhiwa kwa wananchi.

Alitaja mkakati wa usimamizi na uendeshaji alisema ni pamoja na kuunda chombo huru cha watumiaji maji, uendeshaji na matengenezo ya mradi utasimamiwa na wananchi kwa asilimia 100 kwa kuzingatia sera ya maji ya mwaka 2002.

WAZIRI wa Maendeleo ya Nishati na ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi