loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yashauriwa kupunguza kodi kwa viwanda

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya rangi ya Berger Paints International Ltd, Mehbood Bharwan alisema jana kuwa viwanda vingi hapa nchini vimekuwa vikishindwa kujiendesha kutokana na kutozwa kodi kubwa tofauti na uzalishaji.

Alisema ingawa Serikali inahitaji kodi ili kuboresha huduma za jamii, lakini kodi hiyo ni kubwa na inatishia ukuaji wa sekta hiyo.

“Utakuta kiwanda kinalipa kodi zaidi ya tatu kwa wakati mmoja kwa sababu kuna kodi katika mishahara, kodi katika bidhaa na kodi katika usafirishaji ambazo ni kubwa kwa upande wetu,” alisema.

Alisema endapo Serikali itapunguza kodi hizo, viwanda vitaweza kuajiri watu wengi na kuzalisha zaidi na kuweza kusaidia kuinua uchumi wa nchi na wananchi kwa ujumla.

Aidha Mkurugenzi huyo aliiomba Serikali kuboresha miundombinu ya barabara na reli ili kusaidia usafirishaji wa bidhaa zao kwa gharama nafuu.

Alisema bidhaa hizo zikizalishwa kwa gharama nafuu na zikitozwa kodi chache zitasaidia pia kuwafikia wananchi ambao ndiyo walaji kwa gharama nafuu.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Hellen Mlacky

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi