loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yasitisha uagizaji mchele

Colemani alihoji juu ya uagizwaji wa mchele na sukari kutoka nje wakati wa majadiliano baada ya uzinduzi wa ushirikiano mpya kati ya Tanzania na Uingereza. Alisema baada ya kujitokeza tatizo la uhaba wa nafaka nchini, Serikali iliruhusu wafanyabiashara kuagiza tani 120,000 za mchele kutoka nje ya nchi kwa awamu mbili.

“ Kulikuwapo na tatizo la nafaka na ndipo tulipoamua kuagiza mchele kutoka nje kwa awamu mbili, awamu ya kwanza ziliingia tani 60,000, lakini kwa sasa Serikali imesitisha kuagiza awamu ya pili ya mchele,” alisema.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema nia ya Serikali ilikuwa ni kuandoa kadhia kwa wananchi, hasa kutokana na baadhi ya wafanyabiashara kuficha mchele mpaka hapo wanapoona bei ya nafaka hiyo imepanda sana. Kuhusu uagizaji sukari kutoka nje, Chiza alisema Serikali inakusudia kuunda timu itakayojumuisha wajumbe kutoka serikalini, wazalishaji wa sukari na wafanyabiashara, ambao wataangalia suala la uagizaji na bei ya sukari.

Alisema timu hiyo ndiyo itakayosaidia kujua mahitaji na bei halisi ya bidhaa hiyo nchini ili kila upande usiathirike na hatua ya kuagiza sukari nje ya nchi.

“ Hatuwezi kusema kuwa tutapiga marufuku kuagiza sukari nje ya nchi, tunachota ni kuweka uwiano sawa wa kuzalisha na uagizaji wa sukari ili kusiwepo na upande utakaoathirika,” alisema.

Kuhusu upatikanaji wa nafaka ya shayiri kwa ajili ya viwanda vya bia, Chiza alisema kwa sasa Serikali inaangalia uwezekano wa kuzalisha zao hilo Kusini mwa Tanzania.

Alisema kwa sasa itakuwa vigumu kuongeza uzalishaji wa zao hilo katika maeneo ya Kaskazini, kutokana na uhaba wa ardhi.

Majibu ya Chiza yalitokana na swali lililoulizwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha bia cha Serengeti, Steve Gannon alizungumzia uhaba wa shayiri na kukosekana kwa viwanda vya kuchachusha kimea nchini.

Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu alisema Serikali imepanga kuhakikisha inavutia wawekezaji kuwekeza katika viwanda vya kuchachusha kimeo ili kuondoa tatizo la kampuni za bia kwenda kuchachusha kimea Kenya.

RAIS John Magufuli amesema Manispaa ya Ilala imepandishwa ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi