loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yazindua mtambo kuchakata dhahabu

Mradi huo ulizinduliwa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele katika sherehe za uzinduzi wa mradi huo ulioanza kujadiliwa mwishoni mwa mwaka jana.

Wizara ya Nishati na Madini kwa kugundua umuhimu na mchango wa wachimbaji wadogo katika uchumi wa nchi ulibuni mradi huu na kuwashirikisha wadau wengine wa maendeleo wakiwemo WB, migodi mikubwa ya dhahabu na chama cha wachimbaji wadogo na kusaini mkataba wa makubaliano mnamo mwaka 2009.

Kwa upande wake mwakilishi wa Benki ya Dunia, Mamadou Barry alizungumzia utekelezaji wa mradi huo kuwa ni matokeo ya utendaji mzuri wa Serikali ya Tanzania hususan Wizara ya Nishati na Madini katika kutekeleza miradi inayofadhiliwa na benki hiyo hivyo kuifanya benki hiyo kuwa na imani na watendaji wake.

Barry ameeleza kuwa kwa kutambua mchango wa sekta ya madini kwa maendeleo ya Tanzania na kuwa na nafasi kubwa ya kutoa ajira kwa takribani Watanzania milioni moja, ikiwa ni ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, Benki ya Dunia imeona ni vyema kuwaendeleza wachimbaji wadogo ili kuwasaidia katika kukuza uchumi wao.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi