loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yazitaja 'njia za panya'

Inaelezwa kuwa, idadi kubwa ya wafanyabiashara hao, hawatumii tena mipaka ya Namanga (Arusha), Horohoro (Tanga), Sirari (Mara) na mingine yenye ukaguzi wa maofisa wa Shirika la Viwango (TBS) badala yake, wameufanya mpaka wa Mtukula unaoitenga Tanzania na Uganda kuwa njia yao kuu, kwa kuwa mpaka huo, hauna maofisa wakaguzi wa viwango wa nchini.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Maria Bilia alisema juzi kuwa kuifahami mianya hiyo ni hatua kwa TBS kukabiliana na tatizo la kuingizwa bidhaa zisizofaa nchini, kwa sababu itasaidia kujua ni kiasi gani cha maofisa udhibiti na ukaguzi wawekwe kwenye maeneo hayo.

Kwa mujibu wake, idadi hiyo ya njia za panya inaongezeka siku hadi siku, hivyo, kuhitaji mkakati endelevu wa kuimarisha ushirikiano na Jeshi la Polisi, pamoja na Polisi jamii, kwa sababu hata Serikali ikisema iweke wakaguzi katika mipaka yote, wafanyabiashara wasio waaminifu wataanzisha yakwao.

“Ndio maana tunasisitiza elimu kwa jamii ili kila Mtanzania ageuke kuwa polisi jamii kwa kutoa taarifa, kusaidia kukamata na hata kuzuia mbinu za kuingiza bidhaa zisizo na ubora katika soko la Tanzania. Jeshi la Polisi linatusaidia kudhibiti bidhaa hafifu na kwa hatua ya kuanzisha polisi jamii, linastahili pongezi,” alisema.

Katika hatua nyingine, Kaimu Mkurugenzi wa TBS, Joseph Masikitiko alisema juzi kuwa ili waweze kukabiliana na uigizaji bidhaa zisizo na viwango kutoka nje ya nchi, shirika hilo linahitaji angalau watumishi 900 zaidi kwa kipindi hiki.

Hata hivyo, katika jitihada za kulinda soko la ndani dhidi ya bidhaa hafifu kutoka nje, Serikali ilianza kuajiri watumishi mwaka huu, ambapo ilielezwa kuwa, kwa awamu ya kwanza, wataajiriwa 60 kati ya 200 walioombwa kwa kila mwaka, hadi idadi kamili itimie.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi