loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Shein ataka Kifimbo cha Malkia kituzindue

Aliyasema hayo wakati akipokea Kifimbo cha Malkia, Ikulu mjini Unguja na baadaye kutembezwa katika baadhi ya mitaa ya Unguja ikiwemo Mji Mkongwe.

Kifimbo hicho kinaashiria maandalizi ya Michezo ya Jumuiya ya Madola ambayo mwaka huu, itafanyika Glasgow nchini Scotland. Dk Shein alisema wanamichezo wanatakiwa kuandaliwa vyema na mapema ili kushiriki katika mashindano ya ngazi mbalimbali za kimataifa kwa mafanikio makubwa.

“Ni bahati mbaya sana katika miaka ya hivi karibuni tumekuwa tukishiriki katika mashindano mbalimbali ya kimataifa ikiwemo Olimpiki bila ya kupata angalau medali hata moja,” alisema Dk Shein.

Alisema ujio wa Kifimbo hicho uibue changamoto ya wanamichezo kushiriki mashindano kwa kujiamini na kushinda huku akizitaka taasisi zinazoshughulikia michezo hiyo nao kufanya maandalizi ya mapema.

Naibu Waziri wa Habari, Utangazaji na Michezo, Bihindi Hamad Khamis alisema ujumbe mkubwa wa Kifimbo cha Malkia ni kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa watoto ambavyo vinarudisha nyuma maendeleo ya watoto.

Mapema, Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose alisema Michezo ya Madola ni kielelezo cha watu na wananchi wa Jumuiya ya Madola katika mshikamano wao.

Alisema ujumbe wa mwaka huu umetolewa na mwenyewe Malkia wa Uingereza wenye lengo la kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia na kuitaka jamii na familia kukomesha vitendo hivyo.

Aidha, Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, Rashid Abdalla Gulam alisema wakati umefika kwa wanamichezo nchini kuiga mfano na uwezo wa mwanariadha nguli Filbert Bayi aliyevunja rekodi ya dunia nchini New Zealand mwaka 1974 na kuliletea heshima kubwa Taifa la Tanzania.

KLABU ya Simba  imetambulisha  mashindano mapya ya Super  Cup, ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi