loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Sheria ya vileo kurekebishwa

Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Alhabib Fereji wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni, Jaku Hashim Ayoub (CCM) aliyetaka kujua lini Serikali itaanza kutekeleza sheria ya kutenga maeneo yanayotumiwa kwa starehe ikiwemo unywaji wa pombe mbali na makazi ya wananchi.

Fereji alisema Serikali imeweka mikakati kuhakikisha sheria zote zinazosababisha migogoro katika jamii inafanyiwa marekebisho ili kuondoa malumbano.

“Serikali imepokea malalamiko mengi kutoka kwa jamii pamoja na kuwepo kwa wingi wa nyumba za ulevi zilizopo karibu na wananchi ambazo zinatishia kuharibu utamaduni wa watoto,” alisema.

Hata hivyo Fereji alisema wananchi wapo huru kuwasilisha malalamiko yao mbele ya Mahakama ya Vileo kwa ajili ya kupinga maombi ya kuwepo kwa biashara ya pombe katika maeneo wanayoishi wananchi.

Tume ya Marekebisho ya Sheria chini ya Mwenyekiti wake Jaji Bakari Mshibe imeanza mchakato wa kuzifanyia marekebisho sheria mbalimbali ambazo zimesababisha malalamiko zikiwa na mapungufu.

Baadhi ya sheria zinazofanyiwa marekebisho ni pamoja na Sheria ya Vileo pamoja na Sheria ya Mahakama ya Kadhi ya Zanzibar ambayo baadhi ya wanaharakati wametoa malalamiko mengi kutaka irekebishwe.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto ...

foto
Mwandishi: Suleiman Khatib

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi