loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Shila ndiye Redd’s Miss Kinondoni

Shila alinyakua taji hilo baada ya kuwashinda warembo wenzake 15 waliokuwa wakiwania taji hilo pamoja na tiketi ya kushiriki fainali za Miss Tanzania 2014 zilizopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Mbali na Shila kutwaa taji hilo, pia aliungana na mshindi wa pili, Camila John na wa tatu, Queenlatifa Hashim kufuzu kwa fainali ya Miss Tanzania.

Warembo hao wa Redd’s Miss Kinondoni 2014 waliingia jukwaani wakiimba wimbo wa Tanzania Tanzania na baadaye Wimbo wa Taifa kuonesha uzalendo. Warembo walioingia hatua ya tano bora ni Getruda Massawe, Qeenlatifa, Shila, Doreen Bene na Camila.

Shindano hilo lilipambwa na burudani kutoka Bendi ya Malaika chini ya kiongozi wake, Christian Bella pamoja na msanii Young Suma (Kipande) ambao walikonga nyoyo za mashabiki vilivyo.

Akizungumzia matokeo hayo, Redd’s Miss Kinondoni 2014, Maria Shila alisema amefurahi kutwaa taji hilo na ndoto zake ni kufanya vyema pia katika taji la Miss Tanzania na hata dunia hapo baadaye.

“Nilitamani kushinda taji hili, Mungu amekuwa mwema sana na namuomba azidi kunisimamia hata mashindano ya Miss Tanzania nifanye vizuri,” alisema.

Mataji mengine yaliyoshindaniwa na kupata washindi wake ni Miss Photogenic, Miss Talent, pamoja na Balozi wa Hoteli ya Picolo, na Kitwe General Traders.

Hadi sasa zimebaki kanda tatu kufanya mashindano yake kabla ya fainali za Miss Tanzania, ambazo ni Ilala, Temeke na Kanda ya Ziwa.

RUVU Shooting, Kagera Sugar na Gwambina ...

foto
Mwandishi: Mroki Mroki

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi