loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Shule ya msingi haijawahi kufelisha tangu ianzishwe

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo, Mary Mungai wakati wa mahafali ya 14 ya darasa la saba shuleni hapo.

Alisema moja ya sababu ya kutotoa ‘vilaza’ ni ubora wa elimu ambao umeendelea kutolewa shuleni hapo.

“Ni matarajio yetu wanafunzi wote 48 waliomaliza elimu hiyo mwaka huu watafaulu mtihani huo wa darasa la saba, hivyo natoa wito kwa wazazi kujiandaa kuwapeleka katika shule watakazochaguliwa,” alisema.

Alisema shule hiyo ilianzishwa kwa jina la Lusungu Day Care Center mwaka 1994 kama chekechea kabla ya mwaka 1997 kuanza kutoa elimu ya msingi ikisajiliwa kwa jina la Southern Highlands.

“Uongozi wa shule una mipango endelevu ya kuboresha mazingira ya shule ili kudumisha mafanikio tunayopata na kuifanya iwe miongoni mwa shule nyingi zinazofanya vizuri zaidi kitaaluma,” alisema.

Alisema shule itaendelea kutoa mazoezi na mitihani mingi kwa wanafunzi wake ili kuwaimarisha zaidi kitaaluma na kuwaondolea hofu wanapofanya mitihani ya kitaifa.

Alisema katika kuendeleza mikakati yao ya kutoa elimu bora kwa Watanzania wako katika mpango wa kuanzisha shule ya sekondari.

Naye Kaimu Ofisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Nasibu Mengele alisema shule hiyo imekuwa ikiipatia sifa lukuki wilaya hiyo kutokana na mafanikio yake ya kitaalamu ya kila mwaka.

“Tunapozungumza maendeleo ya elimu ya msingi wilayani Mufindi, hatuwezi kufanya hivyo bila kuitaka Southern Highlands. Niwapongeze wanafunzi waliomaliza mwaka huu na ni matarajio yetu watafanya makubwa zaidi ya yale yaliyofanywa na wale waliowatangulia,” alisema.

WASHEREHESHAJI katika matukio mbalimbali zikiwamo sherehe za harusi, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi