loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Shule ya wasioona Kilosa yakabiliwa na changamoto nyingi

Shule hiyo ilianzishwa mwaka 1965 kama shule ya kawaida lakini ilipofika mwaka 1990 kukaanzishwa kituo cha elimu kwa watoto wasioona na wale wenye uoni hafifu, hususan wenye ulemavu wa ngozi (albino). Wanafunzi, walimu na viongozi wa serikali na taasisi za umma waliohojiwa, takriban wote wanakiri kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinaoikabili shule hiyo.

Wengi wanataja shule kukabiliwa na ukosefu wa miundombinu rafiki kwa walemavu, vitabu maalumu pamoja na na uhaba wa waalimu wenye taalum ya kufundisha wanafunzi wenye ulemavu wa kuona. Mkuu wa Kitengo cha Wasioona katika Shule hii ya Msingi Mazinyungu, Ally Mpulu, anakiri kuwepo kwa changamoto zinazowakabili wanafunzi wasioona na wenye uoni hafifu shuleni hapo zinatakiwa kufanyiwa kazi ili kurahisisha mazingira ya kusoma na kujifunzia.

Kuhusu ukosefu wa vitabu maalumu vya kujifunzia na kusomea, Mpulu anasema kitendo hicho kinachochangia kuchukua miaka miwili hadi mitatu kwa wanafunzi hao kuelewa masomo wanayofundishwa shuleni.

“Uhaba wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia unachangia pia kwa mwalimu kumfanya ufundishaji wake kuwa ni mdogo. Wastani wa kufundisha ni wanafunzi watano hadi 10,” anasema Mkuu huyo wa Kitengo. Lingine linalohangaisha kituo, Mpulu anasema ni ufinyu wa bajeti inayotolewa kila mwaka ya shilingi milioni 156 kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kupitia Idara ya Elimu Msingi ambayo anasema haikidhi mahitaji ya uendeshaji wa kituo.

Anasema ni kutokana na ufinyu wa bajeti, uongozi wa shule na kitengo, kuanzia mwaka huu umeanzisha utaratibu wa kuandika barua kwa wazazi na ndugu wa watoto wenye ulemavu kuchangia mahitaji ya wanafunzi. Mahitaji hayo anasema ni pamoja na kuwanunulia sabuni, dawa za maneo, mafuta ya kupaka na nguo za kuvaa shuleni.

Mkuu huyo wa kitengo anasema, hatua hiyo itasaidia kubana matumizi na kuwezesha kiwango kidogo cha fedha kinachotolewa kuhudumia kituo kwa kipindi kirefu katika mambo ya msingi kabla ya mgawo mwingine. Anafafanua kwamba kituo kinahitaji fedha nyingi ili kugharamia chakula kwa wanafunzi wanaoishi bweni, nauli zao kwenda na kurudi shuleni na waalimu wanaowasindikiza, matibabu na kununua vifaa hasa karatasi maalumu za wanafunzi.

Pesa hizo pia zinatakuwa kununua vifaa vya malazi, yaani magodoro, mashuka, vyandarua, ukarabati kwenye mabweni na gharama za umeme “Gharama za uendeshaji zipo juu na fedha inayotolewa haikidhi mahitaji halisi. Karatasi za kuandikia za nukta nundu (braille), kwa mfano, ni shilingi 35,000,” anasema mkuu huyo wa kitengo.

Mpulu anasema wanafunzi wasioona na wenye uoni hafifu kwa sasa ni 74 kuanzia elimu ya awali hadi darasa la saba na kwamba kati yao wavulana ni 45 na wasichana 29. Kuhusu idadi ya walimu wanaofundisha elimu maalumu ni 12. Anasema wanafunzi wanaopokelewa kwenye kituo hicho wanatoka katika wilaya mbalimbali za Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani na Morogoro na kwamba wengi wanatoka kwenye familia duni.

Kuhusu ukusanyaji wa takwimu za wanafunzi wenye ulemavu wa macho wanaopaswa kusoma katika shule hiyo unafanywa kwa kunatumia teknolojia ya kizamani ya ujazaji fomu na kuzituma kwa njia ya posta badala ya kutumia barua pepe na hivyo kusababisha ucheleweshaji wa kuandaliwa kwa taarifa za wanafunzi hao kwa wakati.

Ofisa Takwimu za Elimu wa Mkoa wa Morogoro, Vincent Itambu, anakiri kuwa upatikanaji wa takwimu za ngazi ya mkoa kwa wanafunzi wasioona na makundi mengine kwa wakati ni mgumu. Ofisa Elimu Taaluma wa Mkoa wa Morogoro, MaryRose Kessy, pamoja na kukiri changamoto zilizopo, anasema shule hiyo ya Msingi Mazinyungu ndio shule pekee ya msingi ya bweni katika mkoa wa Morogoro.

Uchunguzi wa mwandishi wa makala haya chuoni hapo uligundua pia kuwepo kwa uhaba wa vyumba vya madarasa. Pia alibaini kuwepo kwa tatizo la maji safi na salama na uzururaji wa mifugo katika eneo la shule. Mbali na mifugo aliweza kuona wananchi wa Kilosa Mjini wakikatisha katika eneo la shule kwa kutumia baiskeli na pikipiki.

Mwandishi aliwakuta baadhi ya wanafunzi wakihangaika kutafuta maji kwa ajili ya kufua nguo na matumizi mengine ingawa kipo kisima kimoja karibu na shule hiyo kilichokuwa hakitoi maji ya kutosha. Pia aligundua kwamba shule haina gari ambalo lingeweza kusaidia huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusomba maji, hususan wakati wa kipindi cha ukame.

Ni kwa mantiki hiyo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatakuwa kuiboresha zaidi shule hii, lengo ikiwa ni kuhakikisha mahitaji muhimu yanapatikana ili shule izidi kutoa elimu bora kwa wanafunzi. Hili linapaswa kuanza kwa wahusika kutembelea shule na kuangalia mapungufu pamoja na kufanyia tathmini bajeti inayopelekwa kwa sasa.

Akielezea umuhimu wa kuongezeka kwa bajeti, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Mazinyungu, Lameck Mkude anasema asilimia 75 ya watoto wenye ulemavu wa ngozi na viziwi wanatoka katika familia zenye kipato kidogo.

Hata hivyo, anasema licha ya shule kuwa na changamoto hizo, maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi wenye ulemavu shuleni hapo ni mazuri ambapo kila mwaka ufaulu ni takriban asilimia 100, ingawa mwaka 2008 ufaulu ulikuwa asilimia 83 na mwaka 2010 ulikuwa asilimia 50.

Lakini anasema watoto watatu waliofaulu darasa la saba mwaka 2011 wameshindwa kuendelea na masomo yao kutokana na wazazi wao kutokuwa na uwezo wa kifedha. Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wenye uoni hafifu wanaosoma shuleni hapo kwa nyakati tofauti wanaelezea matatizo yao mbalimbali ikiiwa ni pamoja na kukosa miwani maalumu ya kuvaa inayokuza herufi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa, Amir Mbaraka, anasema shule hiyo ilipaswa kuwa na uzio ili kupunguza bughudha za watu, mifugo na baiskeli kupita na kuondoa utulivu shleni. Mwalimu Mkuu Mkude naye anasema shule inapaswa kuwa na uzio ambao ni ghjali kuujenga kwani ungesaidia hata ulinzi wa mali za shule “kwa mlinzi mmoja aliyeko hawezi kumudu kuzungukia eneo la shule wakati wa usiku.”

“WANAOFANYA shughuli za maendeleo katika vyanzo vinavyotiririsha maji ...

foto
Mwandishi: John Nditi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi